Kufuatia watu wengi wanapoteza maisha kwa sababu ya kukosa damu wanapopata ajali ili kuweza kuokoa maisha yao na yako mwengewe wananchi wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi wameombwa kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi la kujitolea la uchangiaji wa damu salama kwa hiali.
Wito huo umetolewa na afisa uhamasishaji wa damu salama wilaya ya Liwale,Freddy Magelasa wakati wa zoezi la uchangiaji wa damu salama lilofanyika jana disemba 15 katika viwanja vya stendi kuu ya mabasi wilayani hapa na zoezi hilo litakuwa endelevu.
Afisa uhamasishaji wa damu salama wilaya ya Liwale, Magelasa akizungumza na Liwale Blog amesema moja ya changamoto katika zoezi la uchangiaji wa damu kundi kubwa linaojitokeza ni wanaume ikiwa kundi la wanawake lipo nyuma sana ambapo watumiaji wakubwa wakiwa akimama wajawazito pamoja na watoto na akibainisha kuwa mahitaji ya damu kwa mwezi si chini ya chupa 80.
Kwa upande wao wananchi ndugu Tabibu Mkombozi na Daudi Matumla waliochangiaji damu wamesema wamewataka vijana kujitokeza kwa wingi ili kuweza kuchangia damu salama ili kuweza kuokoa uhai kwa wanaohitaji damu.
Uchangiaji wa damu kwa hiari una faida kwa mtoaji kwa vile unapunguza hatari ya magonjwa ya moyo, kuwepo kwa madini chuma mengi kupita kiasi katika damu kunakodhoofisha utendaji kazi nakuchangia damu mara kwa mara na hurekebisha madini chuma ya ziada katika mfumo wa damu.
faida nyingine ni upimaji wa afya pasipo gharama kwa sababu wakati unapochangia damumtaalamu wa tiba daktari au muuguzi atapima shinikizo la damu yako, mapigo ya moyo na kukufanyia vipimo vya afya bure.
Post a Comment