0

 Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu BAKWATA Taifa na Msemaji rasmi wa baraza hilo,Sheikh Khamis Mataka(katikati) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) jijini Dar Salaam leo wakati akitolea ufafanuzi wa tuhuma tatu zinazoelekezwa kwa Mufti wa Tanzania ,Sheikh Abubakari Zubeir ambazo ameeleza si za kweli.Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Sawa na Tabligh na Msemaji wa Mufti Sheikh Hassan Chizenga na kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu BAKWATA Sheikh Salim Abed.
Mkurugenzi wa Dawa na Tabligh na Msemaji wa Mufti wa Tanzania sheikh Abubakari Zubeir, Sheikh Hassan Chizenga akizungumzia nia njema ya Mufti katika kuwaongoza Waislamu kupitia baraza hilo.Pia ameonya tabia ya Watanzania kusema uongo kwani athari zake ni kubwa katika nchi.


Na Said Mwishehe,Blogu ya Jamii

BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania(BAKWATA)limesema kwa sasa limeimarika kimfumo na kikatiba huku likiweka wazi hakuna chama zozote za kumuondoa Mufti madarakani.

Akizungumza LEO makao makuu ya muda ya BAKWATA Kinondoni Dar es Salaam ,Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu taifa na Msemaji wa baraza hilo, Sheikh Khamis Mataka amesema kinachoendelea sasa ni kuimarisha mifumo kulingana na mahitaji.

Amesema kutokana na mabadiliko yanayoendelea chini ya usimamizi wa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania ,Abubakari Zubeir,kuna watu wanaumizwa na mabadiliko ya mfumo na matokeo yake baadhi yao wanalichafua baraza kwenye mitandao ya kijamii.

Sheikh Mataka amesema wakati baraza likijiimarisha na kufanya mambo makubwa, kuna watu wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kutoa taarifa za kuzusha.Ametumia nafasi hiyo kuwaomba Waislamu nchini kuunga mkono jitihada za Mufti katika kuweka mifumo ambayo italifanya baraza kuwa imara zaidi tofauti na huko nyuma ambako lilingia kwenye matatizo makubwa.

"Kuna mambo mengi yasiyostahili yamefanyika huko nyuma,yakiwamo ya fedha za BAKWATA na mali zake kutumika vibaya.Wapo waliohusika kufanya ubadhirifu huo, wametangulia mbele za haki na hatuna cha kusema zaidi ya kumuachia Mwenyezi Mungu." Tunachoendelea nacho kwa sasa ni kufanya mabadiliko katika maeneo mbalimbali na tunaomba Waislamu kutuunga mkono,tunajua wapo wasiofurahia mabadiliko ya Mufti lakini tutaendelea nayo,"amesema.

Pia amesema kuna taarifa ambazo zinaendelea kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii zikiihusisha BAKWATA.Taarifa hizo ni tishio la kumuondoa Mufti,wafanyakazi walia njaa na mgogoro wa walimu wa shule ya sekondari Bondeni mkoani Arusha inayomilikiwa na baraza hilo.Kuhusu tishio la kumuondoa Mufti ,amesema hazina ukweli wowote na wanafuatilia aliyetoa taarifa.Kuhusu wafanyakazi kudai mishahara ni kweli na hiyo imetokana na malimbikizo ya muda lakini chini Mufti Zubeir wameendelea kulipa.

Amesema malimbikizo yanayodaiwa ni sh Milioni 176 na wanaendelea kulipa.Kuhusu mgogoro haupo kwani ulishaghulikiwa na umepata nafasi kwasababu kuna watu wameondolewa kwa hiyo wanaeneza taarifa mbaya.

Sheikh Mataka amesema BAKWATA ya sasa chini ya uongozi wa Mufti Zubeir ipo imara na kauli mbiu yake yake ya "Jitambue,mabadilika, acha mazoea" imesaidia kuwabadilisha wajumbe mbalimbali wa baraza hilo.Amesema kwa mara ya kwanza wajumbe wa Halmashauri Kuu ya baraza hilo wameshiriki kwenye vikao bila kulipana posho yoyote na miongoni mwa wajumbe walisafiri kutoka mikoani.

Ametumia nafasi hiyo kuelezea hatua ya BAKWATA kuamua shule 10 za baraza hilo kupewa watu binafsi kuzisimamia na zilizobaki zinasimamiwa kwa utaratibu wa zamani.Amesema lengo ni kuangalia mfumo upi unafaa katika kusimamia sekondari za BAKWATA ingawa kuna baadhi ya watu wamezusha sekondari hizo kapewa Mufti jambo ambalo si kweli. 

Post a Comment

 
Top