JESHI
la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia msichana, Elizabeth Benjamini
(20) anayedaiwa kutoa mimba ya miezi minane na kisha kufukia mwili wa
mtoto. Viungo vya mwili wa mtoto huyo vilizagaa hovyo mitaani huku mbwa
wakifanya kitoweo.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa Elias Mwita amethibitisha leo kukamatwa kwa msichana huyo Septemba 9, mwaka huu.
Alidakwa
baada ya jeshi hilo kupata taarifa kutoka kwa raia wema. Askari
walimkamata nyumbani kwake mtaa wa Butengwa, Kata ya Ndembezi Manispaa
ya Shinyanga.
Mwita
amesema katika mahojiano, msichana huyo alikiri kufanya kitendo hicho
na kueleza kuwa katika maelezo ya awali, msichana huyo alieleza kuwa
yeye ni mfanyakazi wa baa iliyopo Manispaa ya Shinyanga.
Alisema bado wanaendelea na mahojiano na baada ya kukamilika, watamfikisha mahakamani kujibu mashitaka yanayomkabili.
Wakazi
wa mtaa huo, Tuma Masanja na Monicka Hassan, walipozungumza na
mwandishi wa habari hizi jana, walisema kuwa baada ya tukio kutokea
hawakufahamu aliyehusika na unyama huo.
Lakini,
baada ya siku moja kupita walishangaa kuona askari wakifika kwenye
nyumba anayoishi msichana huo, aliyefika hapo kumtembelea dada yake,
ambapo katika mahojiano alikiri kutoa mimba ya miezi sita na kufukia
mtoto nje kidogo ya nyumba hiyo.
“Sisi
tulishangaa kuona msichana huyo anaongoza moja kwa moja akiwa
ameambatana na askari eneo ambalo anadai ndio alizika kiumbe hicho,
wakajiridhisha na kumuona hali yake ilivyo kisha wakaondoka naye kwenda
kituoni, lakini dada yake alikuwa akikataa kuwa ndugu yake si mhusika wa
tukio hilo,” amesema Monica.
Mwenyekiti
wa Mtaa huo, Juma Derefa alisema kuwa msichana aliyetupa mtoto na
viungo vyake kuzagaa hovyo mitaani, amepatikana na tayari anashikiliwa
na Jeshi la Polisi, ambapo lilibaini kuwa alikuwa ni mjamzito.
|
Post a Comment