Daktari wake Lisa Bardack amesema kuwa Bi Clinton amekutwa na ugonjwa huo tokea Ijumaa na kuongeza kuwa, Clinton aliongezeka joto na kuishiwa na maji mwilini katika tukio hilo la kuwakumbuka wahanga wa shambulio la Septemba 11.
Baada ya hali hiyo kuokea ghafla, Clinton alilazimika kuondoka mapema, picha zilizowekwa mtandaoni zinamuonesha akisaidiwa na msaidizi wake, huku akitaka kuanguka alipokaribia kwenye gari, lakini baadae bi clinton alitokea kwenye nyumba ya mwanae na kuwaambia waandishi wa habari kuwa anajisikia vizuri.
Awali mgombea Urais kupitia chama cha Republican Donald Trump alionesha wasiwasi juu ya afya ya hasimu wake.
Katika shughuli hiyo majina karibu 3000 ya wahanga wa shambulizi la Septemba 11 yalisomwa.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.