0


Mkuu wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani DCP Mohammed Mpinga amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawapa usalama wa kutosha watoto na kuwazuia wasiende kwenye kumbi za starehe na fukwe za bahari.

Kamanda Mpinga ametoa wito huo leo Jijini Dar es Salaam kwenye mahojiano maalum kuhusu usalama wa watoto hasa kipindi hiki cha Sikukuu ya Iddi ambacho kimekuwa na changamoto kubwa ya watoto kupata majanga kutokana na kukosekana kwa ulinzi wa wazazi na walezi.

Kuhusu usalama barabarani Kamanda Mpinga amepiga marufuku kwa wamiliki wa magari wanaofunga bendera zisizotambulika na jeshi la polisi kuacha mara moja kwa kuwa wanaleta wasiwasi kwa wananchi wengine na wanawahamasisha madereva kwenda mwendo wa kasi kinyume na sheria ya usalama barabarani inavyoelekeza.

Kwa upande wake Kamanda Mstaafu wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Suleiman Kova amewaasa watanzania kuacha matendo ya uvunjifu wa amani ambayo iwapo hayatazuiliwa yanaweza kuleta maafa makubwa zaidi.

Post a Comment

 
Top