Watuhumiwa 10 wa Wizi wa Betri na Vipuli mbali mbali katika minara ya
simu wametiwa mbaroni jana usiku ikiwa ni siku moja tu baada ya Polisi
kwa kushirikiana na makampuni binafsi ya Ulinzi kutangaza kupambana na
wezi wa simu huku zawadi ya fedha taslim ikitangazwa kwa wananchi
watakaosaidia kuwafichua wezi wa Betri hizo.
Watuhumiwa hao 10 walikatwa jana usiku katika maeneo ya Keko magurumbasi na tandika jijini dsm ambapo walikutwa wakiwa na betri tano walizopakia katika gari namba T249 aina ya Noah.
Wakizungumza Viongozi wa kampuni za Ulinzi walioshiriki zoezi hilo la ukamataji wamesema walipata taarifa kutoka kwa wananchi ambapo walifanikiwa kuwanasa watu hao ambapo wamesaidia kuubaini mtandao mkubwa wa wizi wa betri hizo.
Baadhi ya watuhumiwa waliohojiwa na Chanel ten wamekiri kukutwa na betri hizo zilizoibwa katika minara katika maeneo ya tandika ambapo pia wamekiri kushirikiana na baadhi ya watu katika kutafuta wateja ktika maeneo mbali mbali ya jiji.

Post a Comment