0
Eneo iliyotokea ajali septemba 19, 2016 katika barabara ya Liwale kwenda Nachingwea eneo la sheri ya Wangindo katika kata ya Likongowele wilayani Liwale.


Mtu mmoja amefariki dunia aliyefahamika Saidi Mkolaki (21) mkazi wa kata ya Likongowele baada ya kugongwa na pikipiki  septemba 19  wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Kaimu kamanda wa polisi mkoani Lindi,Mohamedi Lipwata akizungumza na Liwale Blog amethibisha kutokea kwa tukio hilo na alisema ajali hiyo ilitokea barabara ya Liwale kuelekea Nachingwea maeneo ya sheri ya Wangindo majira ya saa 2 asubuhi.

Kaimu kamanda wa polisi alisema mwendesha pikipiki namba MC 442 AME aina ya Sunlg iliyokuwa inaendeshwa na Fadhili Limbwilindi (20) mkazi wa kata ya Likongowele alimgonga Saidi Mkolaki aliyekuwa anaendesha pikipiki yenye namba MC 289 AZM aina ya Sunlg na kumsababishia majeraha kichwani kwakuwa hakuvaa kofia ngumu baada ya muda alifariki katika hospitali ya wilaya ya Liwale.

Kamanda Lipwata alisema Fadhili Limbwilindi ambaye majeruhi kalazwa hospitali ya wilaya ya Liwale na alieleza chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi pamoja na  uzembe wa kutochukua taadhali waendesha pikipiki hao bila kuzingatia mtumiaji mwezake aliyegongwa alipinda kuingia sheri bila kuangalia barabaranina aliyemgonga alikuwa mwendo kasi bila kupunguza mwendo.

Kamanda Lipwata ametoa wito kwa madereva wa vyombo vya moto kuzingatia sheria za barabarani kwa kuzingatia alama za barabarani na kuvaa kofia ngumu wakati wote.



KUANGALIA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Post a Comment

 
Top