0
 Ajali ya pikipiki kwa pikipiki kugongana iliotokea leo majira ya saa 2 asubuhi maeneo ya sheri ya wangindo wilaya ya Liwale mkoani Lindi
 Ajali ya kugongana pikipiki kwa kipikipi zenye namba MC 289 AZM na MC 442 AME iliyotokea leo saa 2 asubuhi maeneo ya sheri ya Wangindo wilayani Liwale na kupelea kujeruhi waendesha pikipiki hizo.
Kwa mujibu wa shuhuda Miraji Bandu alisema ajali imetokea majira ya saa 2 asuhuhi leo pikipiki yenye namba MC 289 AZM ilikuwa inatokea Liwale mjini na kujaribu kukata kona kuelekea sheri ya mafuta bila kuangalia mbele huku pikipiki yenye namba MC 442 AME ilikuwa inatokea Liwale B ikiwa inayoosha na barabara na kugongwa.
Baadhi ya mashuhuda ambao hawakuta kutajwa majina yao walisema mwendesha pikipiki namba MC 289 AZM ambayo ilikuwa inatokea Liwale mjini na kutaka kukata kona ndio chanzo cha ajali hiyo wakisema moja ya majeruhi anavuja damu kichwani na amekimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Liwale kwa matiba.

Katika tukio hilo majina ya majeruhi hayakuweza kufahamika mara moja mara baada ya kutokea tukio hilo majerhi hao walikimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
 Askali aliyefika eneo la tukio akiangalia jinsi ya ajali ilivyotikea eneo la tukio
  Wananchi wakiwa eneo la tukio takika Ajali ya pikipiki kwa pikipiki kugongana iliotokea leo majira ya saa 2 asubuhi maeneo ya sheri ya wangindo wilaya ya Liwale mkoani Lindi

 Askari wa usalama barabarani akikagua pikipiki eneo la tukio


Askari wa usalama barabarani akichukua pikipiki iliyopata ajali akiipeleka katika kituo cha polisi wilayani Liwale

Post a Comment

 
Top