SEHEMU YA KUMI
“Vipi
Eddy unamkumbuka yule mdada?”
Aliniuliza
Juma, nikatafari kidogo lakini sikuwa na jibu, nikaamua kumkabili Juma.
“Hapana
mimi nimeshangaa tu, akinishangaa na kunipa pole kwa yalinikuta ila nahisi ile
sura si ngeni machoni mwangu” niliyatoa maneno yale huku nikimtazama kwa makini
Juma. Kabla ya kuibuka na jibu lilionifanya nijione mjinga.
“Wapi
wewe… yule ni Rose rafiki yake mkubwa na Irine,” alisita kidogo Juma huku
akinitazama na mimi nikimtazama katika mfadhaiko.
“Pale
alipokuona ameshikwa na aibu msichana mbaya sana ndugu hafai hata kidogo ndugu,
na kwambia simpendi huyu msichana si mimi tu watu hawamkubali hata kidogo hapa
chuo unavyoona.
Maneno
yale ya Juma yaliniiingia kwenye kichwa changu akili ikaaanza kumtafuta.
“Rose…
Rose!”, kama dakika kadhaa nikakumbuka yeye ndio alikuwaga msaada kwangu mpaka
kujenga mazoea na Irine. Nikaikumbuka
vizuri siku ya kwanza kuonana na Irene kule cafe area yule msichana ndio
alikuwepo pamoja na wenzake wakipiga domo pale karibu na meza nilipokaa mimi.
Oooh!..
aiseeeh!... Juma nimemkumbuka huyu manzi" nilizungumza kwa hamaki.
“Basi ndugu yule msichana hafai hata kidogo….. hafai kaka hata kwa kulumagia…. acha mimi na kwambia acha babu!, mwone vile vile mnafiki tu yule asikuambie mtu ninavyokuambia unavyomuona huyo Irene wako si bure tabia zote unazozijua mbovu yule mdada ndio atakuwa anahusika. Si ndio rafiki yake mkubwa!. Siku hizi wamekuwa hawafai hata kidogo lecture gani asiyewajua hawa we kaulize?!” Juma aliongea kwa msisitizo sana yale maneno yake.
“Basi ndugu yule msichana hafai hata kidogo….. hafai kaka hata kwa kulumagia…. acha mimi na kwambia acha babu!, mwone vile vile mnafiki tu yule asikuambie mtu ninavyokuambia unavyomuona huyo Irene wako si bure tabia zote unazozijua mbovu yule mdada ndio atakuwa anahusika. Si ndio rafiki yake mkubwa!. Siku hizi wamekuwa hawafai hata kidogo lecture gani asiyewajua hawa we kaulize?!” Juma aliongea kwa msisitizo sana yale maneno yake.
Yaliniiingia
vilivyo kwenye ubongo wangu, hapo tena hata hamu ya kutaka kujua habari za Irene
ziliniisha kabisa. Ingetokea wapi?, sikutaka kuutesa moyo wangu kabisa kama
Mungu amenipangia kunipa basi hata nipa lakini si kwa majaribu haya alionipatia
yanatosha kabisa, nilisema na moyo wangu.
Wakati
huo, tulizungumza kwa kina na Juma na nilimweleza juu ya hatima yangu katika
masomo. Uzuri Juma alikuwa rafiki mzuri sana kwangu hakunivunja moyo
alinifaliji, nichukulie hali ile ya kawaida nisifikirie kitu kibaya umri wangu
bado ulikuwa ukiruhusu kizuri sasa nipo na ninafuraha tele na mwenye afya hiko
ndio kikubwa pia hakusita kunipa ushauri juu ya wanawake. Niweze kuwanao mbali
kabisa na kama nitashindwa basi niangalie mwanamke wa kuanae na si wanawake
wote tu. Nilimwelewa vyema na kumwahidi nitazingatia yale yote aliyoniambia.
Hakika
Juma alikuwa rafiki mwema sana kwake, kuhusu yote siwezi kumpa lawama yeye najilaumu mwenyewe na
nafasi yangu.
Muda
nao haukuwa rafiki sana kwetu, baada ya zaidi ya lisaa nikiwa naendelea
mazungumzo. Mida ya kipindi kwa upande
wake Juma ilikuwa ikiwadia hakuwa na jinsi ilimbidi tu aende na kutuacha mimi
na Criss tukiangalia njia ya kutokea ndani ya chuo. Tulipiga hatua kwa dakika
kadhaa huku nikitafakari yale niliyokutana nayo ndani ya chuo kile nikiwa
nimeinamisha kichwa na kukata hatua.
Hamadi
ile na nyanyuaa kichwa kwa mbali niliona kitu, kilifanya mapigo yangu ya moyo
yaende mbio hata nilipojaribu kuizuia hali ile nilishangaa nikishindwa kujizuia.
Moyo
nilihisi maumivu makali kweli, taswira ile niliyokuwa nikiiyona japo kwa mbali
ila haikuwa ikileta hali ya kawaida ndani ya moyo wangu, ili leta mfadhahiko
kwa kiasi hata ule uchangamfu niliokuwa nawo hapo awali njiani mule ulipotea.
Sura
ya Irene mboni zangu ziliweza kusawili kile nilichokuwa na kiona na afadhari
angekuwa yeye pekee yake, bali alikuwa na mwanaume. alivyokuwa amekamatia
vizuri kuino chake. Licha ya yote ila nilishangaa tu roho inauma mbaya. Usiombe
ndugu kitu ukiwa unakipenda haijalishi ikiwe kimekutenda namna gani ila bado
kitabaki ndani ya moyo na kama kidonda ukikigusa basi kina shituka. Basi mimi
nilishituka na ukweli niliumia sana kwa siku hiyo, na kupoteza furaha yangu
kabisa.
Hata
hali ya kuendelea kupita njia ile ilinishinda kabisa miguu yangu ilijikuta
inabadilisha njia huku mikono yangu ikikosa nguvu hata kuishika mikono ya mdogo
wangu Criss.
__________
Nilijivuta
taratibu sikutaka kuungalia hali ile niliyoina kwenye mboni ya macho yangu muda
mfupi, niliendelea kufakamia ardhi taratibu huku kichwani mwangu jambo lile
lilikuwa likinirudia. Hapo sasa maneno ya Juma yalianza kuingia vizuri kwa mara
nyingine ndani ya kichwa changu nakuamini alikuwa sahihi asilimia zote haikuwa
haja tena ya kupinga maneno yake hata kidogo unayapingaje?, kwanza alikuwa
sahihi kabisa Juma kwa kile alichokuwa anakiongea. Hapo niliamini hata ule
msemo wake ya kuwa kama kunavitu duniani hapa havipendeki basi ni viumbe
vinaitwa wanawake.
Mawazo hayo yote yalikuwa yananigonga ni kiwa njiani kurudi
Nyumbani,
hata tulivyoingia nyumbani siku jua nilishaanga tu nipo ndani nimeshika
kidaftari ambacho kilikuwa kama kijitabu nilichonunua wakati tulipokuwa India
na kuanza kuandika mambo yote kuanzia pale nilipoona na yule binti basi kuanzia
hapo niliendelea kuandika tu hata sikujua hali ile ilikuwa ikitokea wapi?.
Naikumbuka
vyema siku ile hatumkuta mama, sikujua alikuwa ameenda wapi kwa muda ule ila
baadae niliweza kufahamu kumbe alikwenda sokoni. Kununua mahitaji na kwabahati
nzuri mama alinunua mboga niliyokuwa naipenda. Ukweli nilifurahi sana na hata
hapo mambo yakitokea chuo kwa siku ile nilianza kuyasahau kwa muda mfupi upendo
wa mama nyie hakuna zaidi yake alikuwa akinifurahisha kweli. Kila siku alikuwa
anapika vitu ninavyo vipenda na uzuri Criss yeye alikuwa kama mimi
ninachokipenda na yeye anakipenda kasoro kwenye mboga ya maharage tu, yeye
alikuwa akiyapenda sana tofauti na mimi .
Sikuchelewa
nilimueleza mama habari za chuo, alinilelewa tu vyema.
************
Zilipita
kama wiki mbili hapo, nilikuwa nahitajika kurudi tena chuoni ilikufatiria
mipango yangu kama nilivyo ongea na mkuu wa shule. Mapema tu asubuhi ya siku ile, nilianza
safari ya kuelekea kule safari hii nikiwa pekee yangu tofauti na mara ya mwisho
nilipoenda maeneo yale.
Baada ya muda kidogo nilifika eneo lile lakini siku ile ilikuwa tofauti kabisa walionekana watu wengi sana wakikatiza chuoni mule namna ya uvaaji wao tu ulitosha kubaini kuwa kulikuwa na bonanza siku ile ndani ya chuo. Sikutaka kufatiria habari zile sana niliendelea kukatiza mitaa kuelekea ofisini kwa mkuu wakati huo tu niliendelea kupishana na wanachuo wengine wakiwa kwenye vikundi vikundi taratibu tu nilipiga hatua zangu ila kunakitu kilinistajabisha, mpaka nikajistukia wakati na pishana na kikundi kimoja cha wadada.
Baada ya muda kidogo nilifika eneo lile lakini siku ile ilikuwa tofauti kabisa walionekana watu wengi sana wakikatiza chuoni mule namna ya uvaaji wao tu ulitosha kubaini kuwa kulikuwa na bonanza siku ile ndani ya chuo. Sikutaka kufatiria habari zile sana niliendelea kukatiza mitaa kuelekea ofisini kwa mkuu wakati huo tu niliendelea kupishana na wanachuo wengine wakiwa kwenye vikundi vikundi taratibu tu nilipiga hatua zangu ila kunakitu kilinistajabisha, mpaka nikajistukia wakati na pishana na kikundi kimoja cha wadada.
Post a Comment