0



                                                 SEHEMU YA NANE

Kwa hasira na uchungu wa hali ya juu nilizidi kutafuta, ila muda wote ule sikuwa naangalia chini ya kitanda. Kitendo cha kuangalia chini ya kitanda hapo ndipo nilipopata kikiona kile kitabu, nikiwa hoi kwa utafutaji ule. Kwa sababu tayari nilikuwa na jambo linaloniongoza sikuijali hali ile ya mwili wangu. Nikiwa na vuja jacho kutokana na saka saka ile. Haraka nilikiwa kodoa macho yangu kwa makini kutafuta ile sehemu haswa niliyoishia.
Nilitaji kusoma neno kwa neno kwa muda huo kana kwamba kama kuna jambo la siri nzito kumuhusu kaka Eddy basi niweze kulitambua mapema. Kama nafsi yangu ilivyokuwa ikitaka kwa muda ule, niliamini uwenda jambo hilo ningeweza kulipata ndani ya kitabu kile kwasasabu fikra zangu zilifahamu kuwa tu kile kitabu kilikuwa cha siri na sidhani kama uwenda mama alikuwa anakijua maana yale yote yaliandikwa na kaka Eddy mwenyewe hayakuwa wazi mwanzoni. Na hata mimi kukipata kile kitabu sikutegemea kuhangahika hangaika kwangu ndiko kulifanya macho yangu yakutane na kile kitabu.
Macho yangu yalikuwa katika ubora wake, baada ya muda kidogo, hatimaye nilifika ile sehemu ambayo nilikuwa nimeishia kuyasoma yalioandikwa ndani ya kitabu kile. Kwa hamasa ya kutaka kujua jambo niliongeza umakini katika macho yangu hapo sasa ilikuwa neno kwa neno.
                                                    ************
Nilimdaka vizuri, kuliko hata walivyokuwa wanategemea hakika, mwili wangu ulikuwa huko vizuri kuliko wakati ambao tulipokuwa tukielekea India.
Nilikuwa mtu mwenye furaha sana, na hata hivyo nao walionekana wakifurahia ujio ule. Tukiwa nyumbani kwa mjomba, tuliandaliwa chakula, kiliongeza furaha zaidi kwa upande wa tumbo langu, ambalo nalo halikuwa limepata vyakula vya kinyumbani nyumbani yaani ya kitanzania kwa muda mwingi.
Baada ya kula chakula pale, huku mimi nikiwa na Criss nikieendelea kumuliza mambo fulani fulani ya kitoto, alionekana akifurahi kila ni nilivyokuwa nikimtupia swali, kiukweli alitukumbuka sana si kidogo.
Mama alizungumza na mjomba kwa dakika kadhaa, alafu tuliaga na kuelekea nyumbani nikiwa sambamba na mdogo wangu Criss. Kutokana hakukuwa mbali sana, kama dakika hamsini hivi tulikuwa tumefika nyumbani.
Tulikaribisha na ukimya pale nyumbani, kwa vyovyote vile ile hali ilikuwa ni lazima tungekutana nayo kwasababu hakukuwa na mtu pale nyumbani tuliishii mimi na mama pamoja na mdogo wangu Criss. Hayo ndio yalikuwa maisha yetu hatukuwa na mfanyakazi kama nyumba za za wanainchi wengi wa Tanzania. Mama hakupendelea suala hilo kwetu kabisa sisi wenyewe ndio tulikuwa tukimaliza kila kitu.
Tuliingia ndani na kuweka mambo sawa baada ya hapo tulilala kwa upande wangu nililala kweli, sijui kwasababu ya uchovu wa safari au la ila nilijikuta tu ninaamshwa na mdogo wangu. Wakati huo jua lilishaanza katika hali ile, sikuamini kana kwamba jua lilikuwa lishaanza kuwaka vile. Taratibu nilijitoa kitandani na kwenda kuoga ilikuweka mwili sawa.
                                       ********
Mazingira hayakuwa yamebadilika sana machoni mwangu baada ya siku chache, niliweza kuzoea hali ya pale. Sikuwa mtembeaji muda mwingi nilibaki ndani. 
Siku zilivyozidi kwenda hali yangu ilizidi kuimalika, na kuwa njema sana wakati huo sikuwa na wazo la mtu anayeitwa Irene, lilifutika kabisa ndani ya kichwa changu. Nilimsahau kwa kiasi kikubwa sana, moyoni mwangu hakuwepo tena mwanamke yule, na sikudhani tena kama angeweza kurudi tena kwenye maisha yangu katika namna ambayo sikujua kama ingenigharimu. 
Niliendelea kumsaidia mama katika miradi yake mbalimbali siku hadi siku. Miradi yake ilionekana kuimalika haswa, na harufu ya pesa ilianza kutunyemerea kama zamani. Hali ambayo ilitufanya tusahau kwamba tulitumia kiasi kikubwa hapo nyuma katika kupambana na afya yangu. Mama alinisifia sana, kwajinsi nilivyokuwa nikipambana na kumpa mbinu mbali mbali ambazo ziliweza kusaidia hali yetu ya kiuchumi kuimalika vizuri, kuliko kawaida. Niliendelea kusimamia kwa makini mno mpaka kipindi ambacho ilinibidi niende chuo kufatiria masuala yangu ya masomo.

Wakati huo karibia mwaka ulikuwa unakatika tangu ya tokee yale. Naikumbuka siku ile niliyopanga kwenda chuo kufatiria mambo yangu nilienda sambamba na mdogo wangu Criss, wakati huo nilikuwa nimeshafanya mawasiliano na Juma ambaye alikuwa rafiki yangu mkubwa na kumpa taarifa kuwa ningefika maeneno yale muda wowote.
Nilipofika mahali pale palikuwa kumebadilika kidogo tofauti na mwanzo. Nilionana na watu wengi kila moja alitukodolea macho kila nilipokuwa na tukikatiza si wadada si wakaka ambao wengi wao sikuwa na fahamiana nao. Nilizidi kusonga mahali ilipokuwa ofisi ya mkuu wa chuo huku nikiwa na mdogo wangu Criss ambaye yeye kazi yake ilikuwa kushangaa tu kila tulipopita ndani ya chuo kile.
 
Moja kwa moja mpaka pale ofisini tulikaa kwa muda kidogo na hatimaye tuliingia ndani kuonana na mkuu yule, kabla sijasema hata kitu mkuu alinena kitu kilichonistua kidogo.

Post a Comment

 
Top