0
Tokeo la picha la WAZIRI NAPE

WAZIRI wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametangaza kuvifungia kwa muda usiojulikana vituo viwili vya Redio kurusha matangazo yao.

Waziri Nape ametangaza uamuzi huo hivi punde katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kuzitaja redio hizo kuwa ni Radio 5 FM ya Arusha na Radio Magic FM ya jijini Dar es Salaam.

Amesema redio hizo kwa nyakati tofauti na katika vipindi vyao tofauti walitangaza habari zilizokuwa na uchochezi ambazo zinaweza kuvuruga amani ya nchi.

Aidha Nape amesema amewasiliana na kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) ili kuwahoji wahusika na kisha kushauri adhabu ambazo zitakazofaa dhidi yao.

Post a Comment

 
Top