0



SEHEMU YA TISA

“Habari zako ninazo kijana wangu mapema tu nilipokea taarifa zako kutoka kwa mkuu wa kitengo chenu hapa chuoni pole sana kwa matatizo kijana wangu”, alisita kidogo huku akiendelea kunitazama nami nikiwa kimya kisha akaendelea kusema. “Maisha yana changamoto sana usimwamini mtu kabisa haswa hivi visichana vya hapa chuo.
Vinatamaa sana havina mapenzi hata kidogo kijana wangu mimi ni kama mzazi kwako lazima nikwambie ukweli kwasababu huku tumepitia sisi, nimefanya kazi hapa muda mrefu hivyo maisha ya chuo kwa jumla usione umri wangu huu na wajua vijana wengi hapa na maisha yao kwa ujumla”. Yule mkuu wa chuo aliongea bila kupepesa macho, maneno  ambayo yalikuwa ni kama mwiba mkali kwangu. Ulikuwa mwiba kweli ambao ulinichoma na kutonesha kidonda changu ambacho kilikuwa kinakaribia kupona kabisa.
Nilimtazama kidogo, nikafumba funda la mate mdomoni mwangu kisha nikamkabili kwa maneno ambayo nilijua yangeweza kubadilisha mada na kulekea kile nilichokuwa nimejia ndani ya ofisi yake,. “Aahh… nimekupata mkuu vizuri sana, kwa sasa nimesahau vitu vyote vya nyuma sasa naangalia maisha yangu maana familia inanitegemea” nilimaliza huku nikiachia tabasamu la kinafiki kwenye mtazamo wake.
Mkuu alinyamaza kimya baada ya maneno yangu, huku akishighulisha mikono yake kupekua pekua mafaili fulani. Hata sikujua alikuwa anataka kunipa nini?,. Mara alitoa karatasi ambayo ilikuwa ni form nakunipatia. Nilivyopewa nilijua niyakuomba kurudia mwaka kutokana na kupitwa masomo.  Jambo lile nilishalitegemea kutokea sikuwa na wasi wasi, nilipokea kwa moyo moja. Kabla ya kunipatia meelekezo juu ya form ile.
Tulitoka nje mimi na Criss nilitulia kidogo nakuanza kuijaza ile form dakika chache niliweza kuijaza vizuri kama inavyotakiwa.  Nikamrudishia mkuu ambaye aliniambia nirudi baada ya wiki ili ile form aipeleke mahali husika. Nilimwelewa mkuu vizuri kile alichotakiwa kufanyika juu ya kuhakisha naendelea kupata elimu yangu.

Tulitoka ofisini na kuanza kukatiza mitaa ya chuo taratibu mpaka ilipokuwepo darasa ambalo nilikuwa nikisoma nilipiga hatua huku nikiwa nimeshika mkono Criss. Hatua kadhaa tulifika darasani mule hakuna aliyeamini kila mwanafunzi wa darasa lile alishikwa na nafuraha isiyo na kifani. Kila moja alifurahi kuniona tena nikiwa kwenye afya njema kabisa hakuna aliyeamini juu ya ujio wangu katika nyakati zile.  Kutokana na kukubalika darasani mule wapo baadhi ya wasichana walikuwa wakilia, vilio vya furaha. Si wasichana tu walikuwa wanafuraha ajabu juu ya ujio wangu hata wavulana nawo nyuso zao zilibeba furaha isiyo na kifani. Furaha ambazo kwa upande wangu niliziona za kawaida maana wachache ndio walikuwa wakijitokeza nyumbani na hata kuwasiliana nami juu ya afya yangu, hivyo niliona kama unafiki tu mbele ya macho yangu lakini sikuonesha wazi wazi.

Nilichofanya nikumchukua rafiki yangu Juma ambaye nilishampa mapema taarifa ya kuwa ningekuwa pale, siku mbili nyuma.
Tulitoka  nje huku tukiendelea kuzungumza, kiukweli tulizungumza  vitu vingi sana. Na hata Juma hakusita kunigusia habari za Irine kipindi chote ambacho mimi nilikuwa sipo vituko vyake.
Hakika na kiri wazi hakuwa msichana ambaye mwanzoni nilidhani bwana ndio amepanga niwe nae, nilimlaumu Mungu kunikutanisha na mwanamke yule huku nikiapa sitaweza kuwa na mwanamke yule hata ingekuwa kwa kushikiwa mtutu.
Tabia zake zilikuwa mbovu sana ndani ya chuo, kila mtu alifahamu nyendo za binti yule.  Namna ambavyo Juma alivyokuwa akiniambia nilihusanisha na namna nilivyokuwa nikiingia chuoni pale kila mtu alivyokuwa akiniangalia hapo nilifahamu vyema kwanini nilikuwa naangaliwa sana hapo awali. Nilijuwa watu walikuwa wananisikitia kuling'ang'ania fupa ambalo lilikosa mlaji, nilijiona mpumbavu muda wote kweli Irene hakuwa msichana wa aina yangu kabisa hakustairi kupendwa na mimi. Juma aliendelea kuongea mengi hakika alienda mbali sana,
 “Ahahh.. hiiiiii”, niling'ata meno kwa hasira, grafla nilisikia sauti ikiwa inaniita jina langu.

Sauti ile ilipenya kwenye ngoma zangu za masikio kudhihirisha ni jina langu lilikuwa likiitwa si mimi tu hata Criss mdogo wangu alikuwa akisikia sauti ile wakati nikiendelea kumsikiliza Juma.
Niligeuza shingo yangu kuangalia ni nani alikuwa akiniita, kugeuka tu mboni zangu zilikutana na taswira ya mdada ambaye sikuweza kumtambua vizuri hadi alipofika mahali pale tulipokuwa mimi Juma na mdogo wangu Criss. Nilimfahamu kwa sura jina lilikuwa limeshanitoka, ni muda mwingi na vile sikuwa sana na mazoea na watoto wa kike, hivyo nilishamsahau jina lake ila sura haikuwa ngeni kabisa.
Muonekeano wa yule binti baada ya kutufikia na kuanza kuzungumza nae niliona vyema hakuwa anaamini ambacho anakiona mbele yake kamwe. Sura yake ilionekana imeshikwa na mfadhahiko mbele ya macho yangu. Niliongea nae dakika chache na kutuacha pale mimi na Juma tukiendelea kuongea jambo. Juma akanitupia swali, swali likaleta dhahama kwenye kichwa changu.

Post a Comment

 
Top