Mtu mmoja na mkewe
kutoka jamii ya Daliti inayobaguliwa tangu jadi nchini India wameuawa,
mmoja akiwa amekatwa kichwa na mwengine kunyongwa kwa kushindwa kulipa
deni la Rupee kumi na tano ambalo ni karibu senti ishirini na mbili tu.
Polisi
kaskazini mwa taifa hilo wamethibitisha kisa hicho ambapo yasemekana
mfanyi biashara anayetokea jamii ya hadhi ya juu,aliwaua wanandoa hao
kwa kushindwa kulipa deni la biskuti walizokuwa wamewachukulia watoto
wao.
Mfanyi biashara huyo amekamatwa.
Ubaguzi kwa misingi ya
kijamii umeenea sana nchini India, huku watu wa jamii ya Daliti
waliokuwa wamebadikwa jina la 'the untouchables' wakiwekwa kwenye daraja
la chini kabisa kwenye sera hiyo ya kibaguzi nchini India iitwayo
'caste' ambapo wananyimwa fursa nyingi za kimaendeleo na hivyo kubaki
katika lindi la umaskini .
Hata hivyo Visa vya ukatili wa kibaguzi
dhidi ya jamii ya Dalit katika jimbo la Gujarat vimeongezeka mnamo siku
za hivi karibuni na vimesababisha wimbi la maandamano kutoka watu wa
jamii hiyo.
Post a Comment