Hatma ya mshindi wa
kombe la dunia Bastian Schweinsteiger katika klabu ya Manchester United
haijulikani kufuatia kuajiriwa kwa kocha Jose Mourinho .
Mourinho tayari amefanya usajili wa wachezaji watatu na sasa anamuandama kiungo wa kati wa Juventus Paul Pogba.Schweinsteiger mwenye umri wa miaka 31,anaonekana kuwa mmoja wa wachezaji tisa ambao huenda wakaihama klabu hiyo.
Kiungo huyo wa kati ambaye ametangaza kustaafu katika soka ya kimataifa alifanya mazoezi pekee wakati ambapo wenzake walifanya zoezi pamoja kwa mara ya kwanza.
Kati ya wachezaji hawa hakuna hata mmoja aliyechaguliwa katika kikosi cha wachezaji 23 kwa mechi ya kirafiki siku ya Jumamosi dhidi ya Galatasaray mjini Gothenburg.
Post a Comment