0
 
Amani nchini Somalia
Soka imefaulu nchini Somalia mwezi huu kile viongozi na wapatanishi wameshindwa kufanya katika kipindi cha miongo miwili.

Timu kutoka maeneo yote zilikutana mjini Mogadishu kushiriki katika mchuano mmoja.

Mchuano huo ulifanyika mjini Mogadishu ,mji mkuu ambapo siasa za mbari huzuka na kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Hatahivyo,mashabiki katika uwanja huo walishangilia timu zao bila kisa chochote kwa zaidi ya siku 12.

Timu kutoka jimbo la Kaskazini mashariki la Puntland iliibuka mshindi katika fainali kwa kupata mabao 5-3 katika mechi dhidi ya jimbo la Jubaland ambayo ilibainiwa na mikwaju ya penalti.

Waandilizi wa mchuano huo wamepongezwa sana hadi kuilazimu idhaa ya BBC Somalia kuanzisha mjadala kuhusu iwapo soka ndio suluhu ya kuleta amani nchini humo .

Post a Comment

 
Top