0
Mohammed Morsi
Mahakama ya Misri imempatia kifungo cha maisha jela aliyekuwa rais wa Kiislamu Mohammed Morsi baada ya kukamilika kwa kesi yake ya upelelezi.
Ni miongoni mwa washtakiwa wanaoshtumiwa kwa kutoa nakala za siri kwa taifa la Qatar.
Wakili wa Bw Morsi amesema kuwa aliwachiliwa huru kwa upelelezi lakini akapewa hukumu hiyo kutokana na kuliongoza kundi haramu.
Wengine ni waandishi wawili wa Aljazeera ambao walihukumiwa kifo wakiwa hawako mahakamani. 
Aliyekuwa rais wa Misri Mohammed Morsi
Hatahivyo kiongozi huyo wa zamani ana uwezo wa kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama unaojiri wakati ambapo sekta ya mahakama ya Misri inaendelea kukosolewa na makundi ya wanaharakati duniani.

Post a Comment

 
Top