Waziri wa utalii
nchini Brazil , Henrique Alves,amejiuzulu siku moja baada ya kushtumiwa
kwamba aliitisha hongo kuchangia kampeni yake kutoka kwa shirika kubwa
la serikali lililo kwenye biashara ya mafuta Petrobras.
Anakuwa waziri wa tatu kujiuzulu kutoka kwa serikali ya rais Michel Temer kutokana na kashfa hiyo.
Hata hivyo bwana Henrique Alves amekana madai hayo ya ufisadi.
Jumatano
,mahakama kuu imetoa ushaidi kutoka kwa mmoja wa wakuu wa Pretrobas,
Sergio Machado ambaye amewahusisha wanasiasa ishirini mashuhuri akiwemo
raisi Temer ambaye pia amepinga kuhusika kwake na harakati hizo zisizo
halali.
Post a Comment