Waziri
wa Kilimo Mifugo na Ushirika Mh. Mwigulu Nchemba akipokelewa
katika ofisi ya Mkuu wa Iringa na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa Mh. Amina
Masenza na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela.
Waziri
wa kilimo Mh Mwigulu Nchemba leo amesikiliza malalamiko ya wakulima wa
Tumbaku na kuwahakikishia zao la tumbaku halitakufa kwani linaleta pato
kwa taifa. Waziri wa kilimo Mh Mwigulu Nchemba leo amesikiliza
malalamiko ya wakulima wa Tumbaku na kuwahakikishia zao la tumbaku
halitakufa kwani linaleta pato kwa taifa.
wakulima
wamelalamika sana uchelewashwaji wa pembejeo, bei duni ikiwemo madaraja
mengi ya mfano kuna madaraja zaidi 72 ya grade za tumbaku kitu ambacho
wakulima wamesema inawaumiza sana kwenye bei.
Pia
wakulima wamelalamika ubadhirifu wa chama cha mtandao (Union) kiitwacho
ITCOJE. Katika ziara hiyo Mh waziri aliambatana na Mrajisi wa vyama vya
ushirika Dr. Rutabanzibwa na Mkurugenzi wa bodi ya Tumbaku Bwana Mushi.
Mh. waziri ameagiza matatizo mengi yawe yametattuliwa kabla kikao cha
bunge hakijaanza.
Mh.
Mwigulu aliwasili kwanza ofisi ya Mkuu wa mkoa na kupokewa na Mkuu wa
Mkoa Mh Amina Masenza na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela.
Mh Masenza alimpa taarrifa fupi ya hali ya Kilimo katika mkoa wa IRINGA.
Wajumbe mbalimbali wa mkutano huo wakiwa katika mkutano
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Ushirika akisalimiana na wajumbe mbalimbali wa mkutano huo.
Post a Comment