0

Mipango ya Rais Magufuli kuendelea kupambana na wabadhirifu wa mapato ya Serikali yameendeela kuchukua sura mpya.
Kupitia Mamlaka ya Mapato TRA Rais aliweza kufanya mabadiliko makubwa ikiwa ni pamoja na kuwaondoa watendaji ambao walihusika katika upotevu wa fedha za umma pamoja na kuwabana wakwepa kodi ambao ni wafanyabiashara wakubwa.
Kingine kilichonifikia leo kutoa  kutoka kwa Kaimu Kamishna mkuu wa TRA Alphayo Kidata ni kuhusu malengo ya ukusanyaji kodi yaliyofikiwa na mamlaka hiyo ikiwa ni baada ya kazi nzuri ya Rais kuwabana walipa kodi ambapo kwa sasa imevuka lengo la ukusanyaji mapato kwa mwezi Desemba ambayo ni zaidi ya trilioni1.4 kwa bara na visiwani.
TRA yavuka lengo la makusanyo ya kodi kwa mwezi..’TRA imevuka lengo la makusanyo ya mwezi Desemba 2015 ambapo ilikusanya zaidi ya trilioni 1.4 kwa Tanzania bara na visiwani ambapo mapato haya ni sawa na ongezeko la wastani wa bilioni 490 kwa mwezi ukilinganisha na wastani wa makusanyo kwa mwezi Julai hadi Novemba ambapo ni bilioni 900′..Kidata HABARI ZAIDI SOMA HAPA
             

Post a Comment

 
Top