Miili ya watu zaidi
mia moja na sitini waliokufa katika ajali ya ndege nchini Misri ipo
njia kuelekea katika mji wa St. Petersburg nchini Urusi.
Katika
ajali hiyo ya ndege iliyotokea siku ya jumamosi huko eneo la Sinai watu
wote mia mbili na ishirini na nne walikuwa katika ndege hiyo walikufa.Rais wa Misri Abdel Fattah al Sisi ametaka watu wote wawe na uvumilivu wakati uchunguzi ukiwa unaendelea.
Mmoja wa wachunguzi wa maswala ya anga kutoka Urusi amesema kuwa ndege ya Urusi iliyoanguka katika rasi ya Sinai nchini Misri ililivunjika ikiwa hewani.
Aleksandr Neradko amesema kwamba mabaki ya ndege hiyo yametapakaa katika rasi ya Sinai.
Abiria wote mia mbili na ishirini na wanne waliokuwa ndani ya ndege hiyo ,ambao idadi kubwa ni raia wa Urusi,wamefariki dunia,naye mchunguzi kutoka nchini Urusi amesem akwamba ni mapema mno kutaja chanzo cha ajali hiyo.
Kikundi cha wanamgambo wa dola ya kiislam mapema wamekiri kutungua ndege hiyo,madai ambayo yamepingwa na serikali za Urusi na Misri.nchini Urusi kulikuwa na siku ya maombolezo.
Post a Comment