Wakenya Stanley
Biwott na Mary Keitany walishinda mbio za wanaume na wanawake katika
mbio za New York Marathon zilizoandaliwa Jumapili.
Biwott
aliponyoka kutoka kwa Mkenya mwenzake Geoffrey Kamworor maili ya mwisho
na kushinda mbio za wanaume kwa kutumia saa mbili na sekunde 34.
Kamworor ndiye bingwa wa dunia wa mbio za nyika.Bingwa wa mbio za Boston Marathon Lelisa Desisa (Ethiopia) alimaliza wa tatu.
Bingwa mara mbili wa London Marathon Keitany naye aliibuka kuwa mwanariadha wa kwanza kuhifadhi taji la New York Marathon baada ya Mwingereza Paula Radcliffe aliyefanikiwa kutwaa taji hilo 2007 na 2008.
Alimshinda Muethiopia Aselefech Mergia na kumaliza mbio hizo kwa muda wa 2:24:25.
Muethiopia mwingine, Tigist Tufa, alimaliza nambari tatu.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto ni miongoni mwa viongozi waliofika mtandaoni kuwapongeza wanariadha hao kwa ushindi wao.
“Jiungeni name katika kuwapongeza Mary Keitany na Stanley Biwott kwa kushinda mbio za New York Marathon leo na Geoffrey Kamworor kwa kumaliza wa pili,” Rais Kenyatta aliandika kwenye Twitter.
Post a Comment