Chama cha AK cha
Uturuki kimepata viti vingi vya bunge vitakavyoweza kudhibiti bunge la
nchi hiyo baada ya kupoteza miezi mitano iliyopita.
Matokeo rasmi
yanatarajiwa kutangazwa kwa siku kadhaa zijazo lakini karibu kura zote
zimeshahesabiwa ambapo chama hicho cha AK kimejikusanyia zaidi ya
asimilia hamsini kutawala bunge.Matokeo hayo yatampa nguvu rais Recep Tayyip Erdogan ambaye aliita kura hiyo kama kura ya amani na ujumbe kwa wanamgambo wa kikurdi na kudai kuwa vurugu haziwezi kuishinda demokrasia.
Chama kinachoungwa mkono na Wakurdi cha HDP kimepata zaidi ya asilimia kumi zilizopigwa.
Katika eneo la kusini mwa mji wa Diyarbakir maafisa wa polisi walipambana na wafuasi wa chama hicho cha Kikurdi. Wandamanaji waliwatupia polisi mawe na mafataki huku polisi nao wakijibu kwa mabomu ya machozi na maji ya kuwasha.
Kufuatia ushindi wa chama chake cha AK Waziri mkuu wa nchi hiyo Ahmet Davutoglu alitoa hutuba ya kitamaduni katika makao makuu ya chama hicho mji Ankara. Davutoglu amesema chake kitaongoza kwa niaba ya Waturuki wote.
Post a Comment