Mwaandishi wetu ,Nachingwea,
Wanachama
wa mfuko wa afya ya jamii(CHF),wilayani Nachingwea,mkoani Lindi wamehakikishiwa
upatikanaji mzuri wa huduma za afya kwa kuanzishiwa chumba maalumu kwenye
hospitali ya wilaya ambacho kitakuwa na waganga ambao watakuwa wanatoa
huduma kwa wanachama hao pekee.
Hayo
yalibainishwa na Kaimu mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya
Nachingwea,Dr.John Sijaona wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wa mfuko
huo kwenye vijiji vinavyozunguka hospitali ya kanisa katoliki ya Mnero ambayo
imeingia mkataba na halmashauri ya Nachingwea kuwahudumia wanachama wa CHF.
Dr.Sijaona
alibinisha kuwa wanachama hao licha ya kuwa na waganga ambao watakuwa
wanawahudumia pia ndani ya chumba hicho kutakuwa eneo la ambalo watapata dawa
hapo hapo na kuwa kuna dawa za kutosha kwa ajili yao.
“Tumejipanga
kikamilifu kuwahudumia hawa wanachama kwani licha ya kuwa na waganga pia chumba
hicho kitakuwa na dirisha la dawa kwa wanachama”alisema Dr.Sijaona.
Aidha
alibainisha kuwa kwenye vituo vya afya na zahanati zote zenye
wanachama kuna dawa ambazo zimetendwa kwa ajili ya wanachama hao ambazo
kila zinapokaribia kumalizika wahudumu wanatakiwa kupeleka maombi kwa mganga
mkuu ambaye atawapatia kutoka kwenye bohari maalumu ambayo imeendaliwa kutunza
dawa za wanachama wa CHF.
Akizungumza
kwenye uzinduzi huo Katibu tawala wa wilaya ya Nachingwea.Saidi Moka amewataka
watoa huduma kuwa lugha mzuri kwa wagonjwa ambao ni wanachama wa mfuko wa afya
ya jamii na wale wa Bima ya afya ili kuwafanya wasijutie kujiunga na
mifuko hiyo.
Alisema
wapo baadhi wa watoa huduma ambao hawazingatii maadili ya kazi yao kwa
kuwatolea lugha chafu wanachama wa mifuko ya bima ya afya hali inayosababisha
wananchi wengi wasijitokeze kwa wingi kujiunga na mifuko hiyo.
Aliwahasa
wakazi wanaozunguka Hosptali hiyo ya Mnero kujiunga kwa wingi kwenye
mfuko huo ili waweze kutumia fursa hiyo ambayo ipo karibu ambapo
awali wanachama hao walilazimika kupata huduma ya matibabu kwenye vituo vya
kutolea tiba vinavyomilikiwa na Halmashauri.
Naye
Mwenyekiti wa kamati ya usimamizi wa hospitali hiyo ya Mnero Baba Ernest
Chikawe alisema kuwa wamejipanga kutoa huduma mzuri za afya kwa wanachama hao
na kuitaka halmashauri kuwaongezea watumishi kwani kwa sasa kunaupungufu mkubwa
wa watumishi hasa madaktari na wauguzi.
Hlmashauri
ya wilaya ya Nachingwea imeingia mkataba na hospitali ya Mnero wa
kuwahudumia wanawake wajawazito,watoto chini ya miaka mitano na wanachama wa
CHF wanaozunguka hospitali hiyo inayomikiwa na kanisa katoliki jimbo lla Lindi
ambapo halmashauri ndio inayolipia gharama hizo.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.