Afisa
Habari wizara ya Nishati na Madini Badra Masudi akizungumza na
waandishi wa habari mkoa wa Lindi na Mtwara kwenye mafunzo ya siku
mbili yaliyoanza leo yanayohusu Gesi na Mafuta
Na Athuman Cnani na Frank Saidi Kilwa
Waandishi wa
habari wa mikoa ya Lindi na Mtwara wameaswa
kuandika kwa kina habari za uchumi wa gesi na mafuta ili ziweze kutoa elimu kwa
wakazi wake itakayosaidia kukuza miradi ya maendeleo iliyoanzishwa na serikali
hapa nchini.
Wito huo
umetolewa na Dimara Tegambwage wakati wa mafunzo ya gesi na mafuta kwa waandishi
wa habari kutoka mikoa ya Lindi na mtwara yaliyoandaliwa na wizara ya nishati
na madini kwa lengo la kuwajengea uwezo wakati wa uandishi wao.
Amesema
kufuatia matukio ya vurugu yaliyotokea mikoa ya lindi na mtwara waandishi wa
mikoa hiyo wamekuwa wakishindwa kuripoti mara kwa mara habari za maendeleo hasa
zile za uchumi wa gesi na mafuta ambayo kwa sasa imekuwa ni rasilimali kubwa kwa
nchi yetu.
Aidha afisa
habari wa wizara ya nishati na madini BADRA MASOUD amewataka wanahabari kuacha
maswali ya kupikwa badala watumie taaluma yao kuhoji na kuandika habari
walizofanyia uchunguzi wa kina.
Awali
mwenyekitii wa chama cha waandishi wa habari
mkoani Lindi Abdulaziz Ahmadi alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu na yatasaidia waandishi kuwajengea uwezo wa
kuandika habari za gesi na madini.
Abdul azizi
aliitaka wizara ya nishati na
madini kuangalia uwezekano wa kutoa mafunzo hayo kwa uendelevu ili
kuwafanya waandishi wa habari mikoa ya Lindi na Mtwara kuandika habari kwa
uzalendo ,ukweli na usahii zaidi
Mafunzo hayo
yanayofanyika wilayani kilwa mkoani Lindiyameandaliwa na wizara ili waandishi
hao waweze kupata uelewa juu ya matumizi na faida za rasilimali gasi na mafuta
baada ya kugundulika mkoani Mtwara.
wanahabari wa mikoa ya Lindi na Mtwara wakiwa mafunzoni
waandishi wa habari Lindi na Mtwara wakiwa kwenye mafunzo ya Gesi na mafuta yanayoendeshwa na wizara ya nishati na madini yanayofanyika mkoani Lindi
Post a Comment