Mkuu wa Wilaya ya Liwale ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Liwale mkoani Lindi,Mh.Sarah Vicent Chiwamba anawatangazia Wananchi wote kwamba Mafunzo ya Jeshi la akiba (Mgambo) Mwaka 2018 yanatarajia kufanyika mwezi wa Saba (7) mwanzoni katika Tarafa ya Liwale ambapo itahusisha Kata zake zote Tatu
Kata hizo ni Liwale Mjini, Likongowele na Nangando ambapo Kata ya Nangando ndio mwenyeji wa mafunzo hayo,
Vijana wote, Wake kwa Waume mnaombwa kujitokeza kwa wingi kushiriki mafunzo hayo bila kukosa. Fomu za kujiunga zitapatikana katika Ofisi za Watendaji wote wa Kata na mwisho wa kujiunga ni Tarehe 30/05/2018 Saa 08:00 Mchana.
Wote mnakaribishwaa.
Post a Comment