0

Jonny EvansHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJonny Evans

Manchester United wanataka kumleta mlinzi Jonny Evans Old Trafford, miaka miwili unusu baada ya kumuuza mchezaji huyo wa miaka 29 kwenda West Brom, lakini Manchester City na Arsenal wanammezea mate. (Sunday Mirror)
Juventus wanaonekana kuwa na nia ya kumuuza mlinzi Alex Sandro lakini Chelsea walioshindwa kumsaini mbrazil huyo msimu huu, wanakabiliwa na ushindani kutoka Manchester City, Manchester United na Paris St-Germain. (Sunday Express)

Jurgen KloppHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJurgen Klopp

Daniel Sturridge ameambiwa anaweza kuondoka Liverpool kwa mkopo mwezi ujao na meneja Jurgen Klopp wakati mchezaji huyo wa miaka 28 raia wa England anataka kujitafutia nafasi katika kombe la dunia (Sun on Sunday)
Meneja wa Liverpool anasema kuwa alishinikizwa na maajenti wake kumsaini Mohamed Salah msimu huu baada ya hofu kuwa wing'a huyo wa Misri wa umri wa miaka 25 alikuwa mdogo sana kuweza kufanikiwa katika Premier League. (Mail on Sunday)

Mohamed SalahHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMohamed Salah

Manchester United wanatathmini ikiwa watatoa ofa ya karibu milioni 30 kwa wing'a wa Bordeaux mbrazil Malcom, 20, mwezi Januari.(Sunday Times)
Manchester City wamemtazama mlinzi wa Augsburg mjerumani Philipp Max, 24, wakati wanataka kujaza nafasi ya mfaransa aliye na jeraha Benjamin Mendy. (Mail on Sunday)
Meneja wa Everton Sam Allardyce analenga kumsaini mshambuliaji wa Crystal Palace mBelgiji Christian Benteke, 27, wakati wa msimu mpya wa kusaini wachezaji wapya mwezi ujao. (Sunday Mirror)

Post a Comment

 
Top