0
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Salim Ahmed Salim leo disemba 17 amewaaga wajumbe Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kumaliza muda wake wa miaka mitano.

Katika salamu zake mwishoni mwa kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika katika ukumbi wa Makao Makuu ya CCM Mjini Dodoma Mhe. Dk. Salim amewashukuru Wajumbe wa Kamati Kuu na Viongozi wakuu wa chama kwa kushirikiana nao katika kipindi chote cha ujumbe wake na pia amempongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. John Pombe Magufuli kwa uongozi uliokiwezesha chama kuimarika.

Mhe. Dk. Salim amesema kazi nzuri inayofanywa na Mhe. Dk. Magufuli imeonesha dhahiri kuyaenzi mambo muhimu aliyoyasimamia Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Mhe. Dk. Salim ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano na kuwa mtiifu kwa Chama na Serikali.

Post a Comment

 
Top