0

Bei ya korosho imepanda kwenye  mnada wa tisa uliofanyika leo disemba 17 katika  Kata ya mkotokuyana wilaya ya  Nachingwea mkoani Lindi.

Mwenyekiti wa  Chama Kikuu cha Runali, Hassani Mpako amesema kwa ghala la Liwale korosho zimeuzwa kwa bei ya juu ni Sh 3,995 na bei ya chini sh 3,930 ukilinganisha na mnada wa nane ziliuzwa kwa Sh 3,875 - 3825 kwa kilo mnada uliofanyika katika kata ya Mikunya wilayani Liwale.

Katika ghala la Nachingwea korosho zimeuzwa kwa bei ya juu ni sh 4060 na bei ya chini sh 4035.




Post a Comment

 
Top