Maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa yamawaua yamewaua takriban watu watano kusini mwa Chile na kuharibu nyumba kadhaa
Watu 15 hawajulikani waliko katika kijiji kilicho mbali cha Villa Santa Lucía kilicho maarufu kwa watalii.
Rais Michelle Bachelet ametangaza hali ya tahadhari eneo hilo.
Maelfu ya watu wamebaki bila umeme na kutengwa kwa kiasi kikubwa na sehemu zingine za Chile.
Sehemu ya bonde ambapo vijiji vipo kilomita 1,100 kutoka mji mkuu Santiago, lilifunikwa na matope kutoka kwa milima iliyo karibu.
Vyombo vya habari vinaripoti kuwa eneo hilo limekumbwa na mvua kubwa isiyo ya kawaida kwa muda wa saa 24 zilizopita.
Watu kadha wamesafirishwa kwa ndege na kupelekwa mji ulio karibu wa Chaitén.
Makundi ya uokoaji yanatafuta manusura.
Post a Comment