Wakulima na wanachama wa chama cha ushirika Chibandu wakifuatilia kwa umakini mkutano uliofanyika novemba 30 katika ofisi ya kijiji cha barikiwa .(picha na Liwale Blog)
Baadhi ya viongozi walioudhulia mkutano wa pili kutoka kushoto ni ndugu Hasani Mpako mwenyekiti wa chama kikuu cha Runali
Wakulima na wanachama wa chama cha ushirika Chibandu wakifuatilia kwa umakini mkutano uliofanyika novemba 30 katika kijiji cha Ndunyungu kata ya Barikiwa
Mwenyekiti wa chama kikuu cha Runali,Hasani Mpako amewataka wajumbe wa bodi wa vya ushirika wilaya za Ruangwa,Nachungwea na Liwale kufanya kazi na kusimamia majukumu yao kwa kuzingatia kanuni na taratibu ili kuweza kuleta ufanisi katika zao la korosho.
Kutokana na msimu huu wa korosho kumekuwa na changamoto mbalimnali ambazo zimejitokeza katika mauzo ya korosho hali iliyopelekea kuwepo kwa malalamiko kwa akulima.
Ndipo Liwale Blog na mashujaa fm ilitaka kufahamu zaidi majukumu yanayofanywa na mwenyekiti wa chama kikuu cha runali katika kutaua changamoto za wakulima na kuamua kuhudhuri kwenye mkutano wake alioufanya katika kijiji cha barikiwa na ndunyungu katika kata ya Barikiwa wilayani Liwale ambapo alikutana na wakulima wa korosho pamoja na wanachama wa chama cha ushirika cha chibandu.
Ambapo katika mkutano huo lengo lilikuwa ni kukusanya maoni na changamoto wanazokumbana nazo ili kuweza kuzitolea ufafanuzi.Sambamba na hilo mwenyekiti wa runali alitolea ufafanuzi wa kazi ambazo zinatakiwa kufanywa na wajumbe wa bodi.
Mpako alisema kazi kuu ya wajumbe wa bodi ni kuwasimamia wakulima wanapoleta korosho zao kwenye kituo cha ghala ikiwa kukagua na kujiridhisha korosho zinazoletwa kama ni bora ndipo anaandikiwa stakabadhi.
Aliongeza kusema kuwa wajumbe wanafanya kazi kwa mazoea hali inayopelea kuibuka na changamoto kwa kukosa misingi awali na kupelekea usumbufu unaojitokeza kwenye ghala kuu ikiwata kuchambua ili ziwe na sifa na kuingizwa kwenye mnada.
Na Kutokana na vitendo vya makalaani baadhi kutokuwa waadilifu katika utendaji wao wa kazi mwenyekiti wa runali ndugu mpako ametoa onyo kali dhidi yao huku akionyesha kukasirishwa na vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na makalaani hao kwa kujiandikia vyeti hewa na baadae kupelekea wengine kukosa stahiki zao.
Kwa upande wao baadhi ya wakulima akiwamo ndugu Ali kamuna na Abdulah Makanwa walisema kuwa ujio wa mwenyekiti huo kwa kuwaelimisha uwe endelevu kwani wakulima wengi hanakosa elimu ndio maana kunajitokeza na changamoto kwa kukosa misingi awali.
Pia waliiomba serikali kuwapatia wataalumu ili kuweza kuwaelimisha juu Ya matumizi sahihi ya dawa ya korosho na kuwataka wakulima kupanda miche bora ya mikorosho ili kuweza kuzalisha korosho bora na kuongeza uzalishaji.
Post a Comment