0


KAMATI Maalum ya kuzisaidia nchi tano zitakazoiwakilisha Afrika kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Urusi imekubaliana kuwapa wawakilishi hao wote dola za Kimarekani 500,000 kila moja.

Kamati hiyo iliundwa katika kikao chake cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika Novemba 16, mwaka huu mjini Rabat, Morocco chini ya Makamu wa kwanza wa Rais wa CAF, Kwesi Nyantakyi.
Kamati hiyo inayoongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF, Kalusha Bwalya na Marais wa Vyama vya Soka vya nchi tano zilizofuzu Kombe la Dunia mwakani imefikia hatua huyo baada ya kikao chake cha mjini Moscow, Urusi kuelekea upangaji wa ratiba ya Kombe la Dunia Desemba 1, 2017.
Mohamed Salah ni shujaa wa Misri kufuzu Fainali za Kombe la Dunia mwakani Urusi

Fedha hizo ni maalum kuzisaidia maandalizi timu hizo kabla ya kuingia kwenye michuano ya mwakani nchini Urusi. 
Pamoja na hayo, CAF itazisaidia vifaa nchi zote wawakilishi wa Afrika kwenye Kombe ka Dunia, ambazo ni Misri, Morocco, Nigeria, Senegal na Tunisia.

Post a Comment

 
Top