Mpanda mijengo mirefu ambaye ni maarufu sana nchini China amefariki akionyesha moja ya ujuzi wake hatari.
Wu Yongning alikuwa amejizolea maelfu ya mashabiki kwenye mtandao ya kijamii wa Weibo, kutokana na video zake fupi za kutisha akiwa juu ya majengo marefu bila ya kuchukua tahadhari zozote za kiusalama.
Wasi wasi uliwaingia mashabiki wake wakati aliacha kuchapisha video zake mwezi Novemba.
- Jiwe kubwa linalocheza nchini Tanzania
- Mzee mwenye watoto 70 na wajukuu 300 Tanzania
- Pacha waliotungwa siku tofauti Australia
Sasa imeibuka kuwa alikufa baada ya kuanguka kutoka jumba la ghorofa 62 kwenye mji wa Changsha.
Vyombo vya habari nchini China vinasema kuwa alikuwa akishiriki kwenye mchezo wa kushinda pesa nyingi.
Post a Comment