Harambe Stars ya Kenya wabeibuka mabingwa wa kombea la Cecafa Senior Challenge la mwaka 2017 baada ya kuwashinda Zanzibar kwa mabao 3 : 2 kwenye mechi ya kufana iliyochezewa disemba 17 uwanja wa Kenyatta mjini Machakos nchini Kenya.
Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya mabao mawili katika muda wa kawaida wa dajika 90. Kisha mechi ikaongezwa muda wa ziada wa dakika 30 ambalo hakuna timu iliona lango la mwingine.
Baada ya muda wa ziada kumilika mechi kisha ikaingia mikwaju ya penalti ambapo kila upande ulipewa penalti tano za kupiga.
Zanzibar ilipoteza penalti tatu kati ya tano ilizopewa ikimaanisha kuwa ilivuna mabao mawili tu kutoka kwa penalti hizo huku Kenya ikifunga mabao matatu kutoka kwa penalti tano na kupotea moja na kukosa kupiga penalti moja mwisho baada ya Zanzibar kumaliza kupiga penatli zake zote.
Harambee Stars ilishehereka baada kukabidhiwa kombe la Cecafa Senior Challenge katika halfla iliyohudhuriwa na makamu wa rais wa Kenya William Ruto.
Post a Comment