Chama tawala cha Afrika Kusini ANC kimewapitisha wagombea wawili wanaowania kumrithi Rais Jacob Zuma katika uongozi wa chama.
Wagombea hao ni makamu wa rais Cyril Ramaphosa na waziri wa zamani Nkosazana Dlamini-Zuma, mke wa zamani wa bwana Zuma.Kumekuwa na mvutano, hisia zikipanda, wajumbe wakipiga kelele kupinga taratibu za upigaji wa Kura.
Uwaniaji madaraka umeleta mvutano mkubwa wa kisiasa, hali inayoleta hofu kuwa ANC inaweza kugawanyika kabla ya uchaguzi wa 2019.Rais Zuma ameonya kuwa chama kiko hatarini na kiko kwenye njia panda.
Zaidi ya wajumbe 5,000 wanashiriki katika mkutano wa siku nne katika Ukumbi wa Expo Centre mjini Johannesburg.
Kwa namna inavyoonekana, Bwana Ramaphosa ana wafuasi 1,469 kulinganisha na 1,094 wa mke wa zamani wa Rais Zuma, Bi Dlamini-Zuma.
Lakini wengi wanasema pale ambapo matokeo yatawekwa wazi, kunaweza kuwa na tofauti nyembamba kabisa kati ya atakayeshinda na atakayeshindwa yatawekwa wazi, anaeleza Lebo Diseko mwandishi wa BBC aliyeko katika eneo la mkutano.
Rais Zuma ambaye amekuwa mamlakani tangu mwaka 2009 anategemewa kusalia hapo hadi uchaguzi wa taifa mwaka 2019. Afrika Kusini ina ukomo wa rais kwa vipindi viwili vya miaka mitano.
Post a Comment