0
Viongozi wa vyama vya ushirika wakiwa kwenye kikao cha kwenye kikao cha tathumini kwa vyama vya ushirika kilichoitishwa na mbunge wa jimbo la Liwale,mhe. Zuberi Kuchauka kilichofanyika novemba 29kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya ya Liwale

 Mbunge wa jimbo la Liwale,mhe. Zuberi Kuchauka


Viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika wilaya ya Liwale mkoani Lindi walalamikia kupunjwa kwa idadi ya kilo kwenye mizani iliyopo kwenye ghala kuu wakati wanapozifikisha  korosho kwa ajili ya mnada.

Malalamiko hayo yameelezwa novemba 29 kwenye kikao cha tathumini kwa vyama vya ushirika kilichoitishwa na mbunge wa jimbo la Liwale,mhe. Zuberi Kuchauka kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya ya Liwale.

Mapato Mwanja mwenyekiti wa chama cha ushirika Kinali alisema kuwa tatizo la kupunjwa idadi ya kilo kwenye mizani iliyopo kwenye ghala kuu lililopo ghala kuu hapa Liwale limejitokeza msimu huu na suala hilo msimu wa mwaka jana halikujitokeza.

Mwanja akitolea maelezo alisema kuwa suala hilo kwenye chama chake aliwahi kupeleka korosho tani 40 baada ya kupima kwenye mizani hiyo inayolalamikiwa ilionesha zimepungua kilo 760 nae Hashimu Mpegeja kutoka chama cha ushirika Chiluli alisema alipopeleka tani 10 zilipungua kilo 25.

Viongozi hao waliomba suala hilo litafutiwe ufumbuzi haraka na suala hilo Mbunge mhe.Zuberi Kuchauka pamoja na mkurugenzi wa halmashauri ya Liwale bwana Justin Monko watalifanyia kazi haraka ili kubaini chanzo cha tatizo na kulipatia ufumbuzi.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Liwale aliwataka viongozi wa vyama vya ushirika wanapopima mizigo yao kwenye ghala kuu wahakikishe wanapima mzigo baada ya gari jingine limetoka eneo la mizani na wahakikishe kabla ya kuweka mzigo mizani isome alama sifuri (O).

Katika kikao hicho mbunge mhe.Kuchauka alibaini baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika wahafanyi mawasiliano ya mara kwa mara na wakulima ndio maana kunakuwa na malalamiko pia aliongeza kusema kuwa hatima ya ubora wa korosho utategemea na utendaji mzuri wa viongozi kwenye vyama vyao kwa kuwasimamia walima.

Mwenyekiti wa chama kikuu cha Runali, Bwana Hasani Mpako akisoma taarifa alibainisha kuwa vyama vyote vilivyouza mnada namba 2 na 4 vimeingiziwa fedha kwenye akaunti za vyama.

Baadhi ya viongozi wa vyama libainisha kuna baadhi ya wakulima walipopima korosho zao hawakuleta akaunti namba na wengine akaunti zao zilikuwa na matatizo hazisomi na  kuitwa na kuwapa utaratibu wa kuzifanyia maboresho ili kuweza kulipwa na zoezi hilo linaweza kuchukua muda wa zaidi ya siku 2.


Pia katika kikao hicho kulielezwa na kuwepo kwa  changamoto ya usafiri wa kutoa korosho kutoka kwenye vyama kupeleka kwenye ghala kuu hali inayopelekea baadhi ya wakulima kusogea kwenye mnada ndipo viongozi wa vyama waliposhauriwa iknapotokea hali kama hiyo kufanya mawasiliana na wakulima ili kuwaweka wazi ili kupunguza malalamiko.

ANGALIA VIDEO YA TAARIFA YA MWENYEKITI WA CHAMA KIKUU CHA RUNALI

Post a Comment

 
Top