Wafanyabiashara wa soko kuu Lindi mjini wamegoma kufungua soko wakishinikiza kumkataa Mtendaji wa kata kwa kitendo cha kuwa mbabe ,kuwabambikia madeni ya ushuru na kutotoa risiti za malipo ya ushuru
Akizungumzia
tukio hilo Mwenyekiti wa soko Mohamedi Matika alisema wameamua kufunga soko kwa lengo la kushinikiza uongozi wa Manispaa kumwondoa mtendaji wa kata kwa kuto toa ushirikiano kwa wafanyabiashara ubabe na kutotoa risiti za ushuru na faini zinazotozwa kwa wafanyabiashara.
Matika Aliongeza kuwa pamoja kuwa wanalipa ushuru lakini huduma za kijami ikiwemo vyoo, usafi haufanyiki katika eneo la soko jambo ambalo wanadai kuwa faida ya kulipa ushuru haina maana kwenye soko hilo.
Kwa upande wa mtendaji wa kata ya Matopeni Omary Salumu Nyemba amekataa tuhuma hizo na kueleza kuwa wafanyabiashara hawataki kufuata utaratibu na kanuni zilizowekwa na manispaaa za kufanya usafi na kulipa ushuru kwa hiari
Nyemba aliongeza kuwa kitendo cha kusimamia sheria na kanuni mara kwa mara kimetengeza mazingira ya watu kumchukia na kutoa kauli zisizo faa kwake kwa lengo lakumtaka kumzofisha kiutendaji
Nae kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Lindi Injinia Endraw Mayombo alikiri kutokea kwa tukio la kufungwa kwa soko hilo na kueleza kuwa wamewaomba viongozi kufungua soko ili wananchi waendelee kupata huduma na kuwataka viongozi wa soko kukaa pamoja na ofisi yake kujadili suala hilo sambamba na kuwataka watendaji waliokusanya ushuru kurejesha fedha kwa wafanyabishara hao.
Post a Comment