0


Ligi ya Alizeti cup kituo cha Liwale mjini.
Timu ya kigamboni fc yashika nafasi ya 3 na kutinga hatua ya 8 bora baada ya kuichapa timu ya The youth fighter fc mabao 3-1 mchezo uliochewa uwanja wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi.


Timu ya the youth fighter fc ilikuwa ya kwanza kufumania lango la kigamboni fc mapema dakika ya 10 lilifungwa na Jackson Androd.

Magoli ya Kigamboni fc yakifungwa na Sefu Mbundi dakika ya 16 na Dickson Fidels akiiandikia kigamboni fc magoli mawili aliyofunga dakika ya 18 na 43.

Katika kipindi cha pili hakuna timu iliyoweza kuongeza goli kwenye lango la mwezake.
Octoba 6 kutakuwa na mchezo wa fainali wa kukata na shoka kati ya mabingwa watetezi wa ligi ya Alizeti cup timu ya Hawili fc Vs Mitumba fc.

Post a Comment

 
Top