Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai
Taarifa ya Kamati Maalum ya Bunge ya Kuchunguza Biashara ya Tanzanite na
Almasi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2017.
Katikati ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.(Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kupokea Taarifa ya Kamati
Maalum ya Bunge ya Kuchunguza Biashara ya Tanzanite na Almasi kwenye
viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2017.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Spika wa Buge, Job Ndugai baada ya
kukabidhiwa na Spika Taarifa ya Kamati Maalum ya Bunge ya Kuichunguza
Biashara ya Tanzanite na Almasi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma
Septemba 6, 2017.
Spika
wa Buge Job Ndugai akizungumza baada ya kupokea Taarifa ya Kamati
Maalum ya Bunge ya Kuchunguza Biashara ya Tanzanite na Almasi kwenye
viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2017.
Baadhi
ya wajumbe wa Kamati Maalum iliyoundwa na Spika wa Bunge Job Ndugai
kuchunguza Biashara ya Tanzaniate wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kukabidhiwa na Spika wa Bunge
Job Nduga Taarifa hiyo kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba
6, 2017.
Baadhi
ya Wabunge walioshiriki katika hafla ya kupokea Taarifa ya Kamati
Maalum ya Bunge ya Kuichunguza Biashara ya Tanzanite na Almasi kwenye
viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2017.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto kwake)
wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati Maalum iliyoundwa na
Spika ya Kuchunguza Biashara ya Tanzanite baada ya Spika kupokea
Tarifa hiyo na kumkabidhi Waziri Mkuu kwenye Viwanja vya Bunge mjini
Dodoma Septemba 6, 2017. Aliyekaa kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt.
Tulia Ackson na aliyeka kulia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Job
Ndugai.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto kwake)
wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati Malum iliyoundwa na
Spika Kuchunguza biashara ya Almasi baada ya Spika kupokea Taarifa
hiyo na kumkabidhi Waziri Mkuu kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma
Septembea 6, 2017. Aliyekaa kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia
Ackson na aliyeka kulia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Job Ndugai.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amepokea ripoti mbili za kamati ya Maalumu ya
Bunge ya kuchunguza biashara ya madini ya almasi na tanzanite na kuahidi
kuiwasilisha kwa Rais Dkt. John Magufuli kesho asubuhi.
Pia
amesema Serikali haina mchezo katika usimamizi wa rasilimali za Taifa,
hivyo amewataka viongozi na watendaji wote waliokabidhiwa dhamana ya
kusimamia sekta ya madini hakikisha wanatimiza vyema wajibu wao.
Waziri
Mkuu amepokea ripoti hizo leo (Jumatano, Septemba 6, 2017) kutoka kwa
Spika wa Bunge, Bw. Job Ndugai ambaye alikabidhiwa ripoti hizo na
Wenyeviti wa kamati Bw. Mussa Zungu (Almasi) na Bw. Dotto Biteko
(Tanzanite).
“Kesho
saa 4.30 asubuhi nitaziwasilisha ripoti hizi kwa Mheshimiwa Rais Dkt.
Magufuli. Hakuna ucheleweshaji katika jambo hili na Mheshimiwa Spika
(Job Ndugai) kesho twende tukakabidhi wote.”
Waziri
Mkuu amesema kamati hizo zimefanya kazi nzuri na kwamba Serikali
inaimani na ripoti hizo na ushauri uliotolewa utawezesha Taifa
kunufaika na rasilimali zake, hivyo mapendekezo na hoja zote
zilizoibuliwa zitafanyiwa kazi katika kipindi kifupi.
Amesema
taarifa hiyo zimewasilishwa katika kipindi muafaka na zimeonyesha
dhamira ya dhati ya Bunge, kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Magufuli
na Serikali yote kwa ujumla katika kulinda rasilimali za Taifa.
“Watanzania
ni mashahidi kwamba Mwenyezi Mungu ameijalia Tanzania utajiri wa
rasilimali za kila aina. Tunayo ardhi yenye rutuba, madini ya aina
mbalimbali na mengine hayapatikani katika nchi nyingine isipokuwa
Tanzania tu kama vile Tanzanite.”
Amesema
ni lazima rasilimali hizo zisimamiwe na kutunzwa vizuri ili ziwezeshe
kuboresha hali na maisha ya Watanzania wote na kila mwananchi ana jukumu
la kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuleta mageuzi katika Sekta
ya madini nchini.
Waziri
Mkuu amesema suala la kusimamia rasirimali za nchi ni la Watanzania
wote kama ilivyoainishwa kwenye ibara ya 27 ya Katiba ya Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania, ambapo aliinukuu Ibara hiyo kama ifuatavyo:
“27
(1) kila mtu ana wajibu wa kulinda mali asilia ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote inayomilikiwa kwa
pamoja na Wananchi na pia kuiheshimu mali ya mtu mwingine.
“(2)
Watu wote watatakiwa na Sheria kutunza vizuri mali ya Mamlaka ya nchi
na pamoja vita aina zote za uharibifu na ubadhilifu na kuendesha uchumi
wa Taifa na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio
waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao.”
Kamati
hizo zilipewa jukumu la kutathmini mfumo wa uchimbaji, usimamizi,
umiliki na udhibiti wa madini ya Tanzanite na Almasi Nchini, ambazo
zimeishauri Serikali kuhusiana na mfumo bora wa uendeshaji na udhibiti
wa biashara ya Tanzanite na Almasi nchini.
Post a Comment