0


                       

 Na Mwandishi wetu

WANAFUNZI  17524 wa  shule  479   za mkoa  wa  Lindi wanatarajia   kufanya mitihani ya  kuhitimu elimu  ya msingi  tarehe 6 na  7  2017.

Akizungumza  na  timu ya  waandishi wa  habari  Afisa   Habari mkoa  wa Lindi  ERIBARIKI  MAFOLE kwa niaba ya  Afisa  elimu  mkoa WENGI MCHUCHURI  alisema wanafunzi waliosajiliwa 15283 wavulana 7109 na wasichana 8174.

Mafole  alisema wilaya  ya Liwale wanafunzi 2200, Kilwa 4038, Nachingwea  wanafunzi 3599, Lindi 3635 ,  Lindi Manispaa  wanafunzi 1537 wilaya  ya  Ruangwa  wanafunzi 2495.

AIDHA  Mafole  aliwataka  wazazi  na walezi  kuwapa  ushirikiano  kwa watoto  na  kuacha  tabia  ya kuwataka  kutofanya  vizuri  kwenye Mitihani  yao.

Post a Comment

 
Top