Jeshi la polisi mkoa wa mjini magharibi limemkamata kijana
aliedaiwa kumchoma moto mpenzi wake na kumsababishia majeraha makubwa mwilini.
| Add caption |
Tukio
la kukamatwa kwa kijana huyo linajiri siku moja baada ya waziri mwenye dhamana
ya maswala ya wanawake mh: moudline castiko kuomba vyombo vyenye dhamani
kulifanyia uchunguzi suala hilo.
Hapo
jana waziri wa kazi,uwezeshaji,wazee,wanawake
na watoto
Mh:Modelin Castico alimtembelea ndugu Samira Abbas
Ameir alieunguzwa na moto na mpenzi wake katika
hospital ya kivunge
ya koteji makunduchi kusini
Unguja.
Akiwa
hospitalini Mh: Castico amesema Serikali
ya mapinduzi Zanzibar haitolifumbia
macho tukio la kuchomwa moto kwa binti huyo na sheria
lazma ichukue mkondo wake.
Aidha amevitaka vyombo husika
vya ulinzi na
usalama, wanasheria na watu wote
wanaotetea haki za
wanawake kushirikiana ili
kupunguza vitendo hivyo.
Kwa upande
wa majeruhiwa huyo mwenye umri wa
miaka 26 ambae
ni mkaazi wa
Paje kusini Unguja
amesema kisa cha tukio
hilo ni baada ya kumtamkia mpenzi wake huyo kua kamchoka
na anataka kurudi
kwao.
Post a Comment