Waziri wa elimu na mafunzo
ya amali zanzibar mhe Riziki Pembe Juma amewataka walimu
wakuu kuwahamasisha wanafunzi wao kupenda kusoma masomo ya sayansi
na kuwafanya waondoe dhana ya kwamba masomo hayo ni
magumu. .
waziri wa elimu zanzibar Riziki Pembe Juma
Ameyasema hayo wakati akifungua
Mkutano Mkuu wa nne wa Jumuiya ya walimu wakuu Zanzibar (JUWASEZA) ambapo amesema sio jambo la busara kwa
mwanafunzi kuchagua masomo wakati akiwa skuli za sekondari , na kufahamisha
kwamba kitendo hicho kimechangia kushuka kiwango cha ufaulu wa wanafunzi katika
skuli za Unguja na Pemba.
Sambamba na hilo amewataka walimu
wakuu kuacha kujihusisha na masuala ya siasa sehemu za kazi kwani wanaweza
kusababisha kuzorotesha ufanisi wa kazi ya kuwaandaa vijana kuweza kukabiliana
na changamoto za utandawazi.
Mapema Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini
Pemba Omar Khamis Othman amepogeza hatua zinazochukuliwa na Jumuiya ya Walimu
Wakuu Wa Sekondari Zanzibar katika kuzipatia ufumbuzi changamoto za Elimu
na kuahidi kwamba Serekali ya Mkoa itaendelea kushirikiana na Jumuiya
hiyo.
Nae Katibu mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Amali Zanzibar bi Khadija Bakar Juma
amewataka Walimu Wakuu kuwa chanzo cha Maadili, Uwajibikaji na ufundishaji ili
kuongeza idadi ya ufaulu wa Wananfunzi
Post a Comment