Wanaccm nchini wamewatakiwa kujiweka tayari katika kuandikisha daftari
la kudumu la wapiga kura katika Majimbo mbali mbali Zanzibar muda utakapowadia.
Akizungumza
katika ziara ya kuhimiza uhai wa chama mkoa wa kaskazini Unguja katibu wa kamati
maalum ya nec wa idara ya itikadi na uenezi mh: Waride Bakari Jabu pia
amewataka viongozi wa Wilaya kuweka takwimu sahihi ya orodha ya wanachama
katika daftari la wanachama wa Chama Cha Mapinduzi.
Sambamba
na hayo mh: Bi Waride amesisitiza haja kwa wanachama kuendeleza upendo, umoja
na mshikamano wa dhati miongoni mwao na kuwa makini zaidi katika
kufuatilia minendo ya ndani na nje ya chama.
Aidha
amewataka wanaccm kushirikiana baina ya wanachama katika ngazi ya Tawi ili
kupanga mikakati itakayoleta ushindi mkubwa katika uchaguzi
wa mwaka 2020.
Pia
amewataka wanachama wa Matawi husika waishi kwa furaha kwa ushindi wa kishindo
wa katika nafasi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na
Rais wa Zanzibar, Ubunge, Uwakilishi na Udiwani.
Katika
hatua nyengine mh: Waride amewataka wanaCCM wajiandae na Uchaguzi wa kutafuta
uongozi wa Chama 2017 na kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbali mbali ili
kuwapata viongozi walio bora.
Halikadhalika
amewasihi wanachama kujiepusha na vitendo vya rushwa na udanganyifu katika
kutafuta uongozi ndani ya chama hicho.
Aidha
amewakumbusha viongozi kuwaeleza wananchi juu ya mambo yote ambayo
yametekelezwa kupitia Serikali pamoja na viongozi wa Majimbo kama Wabunge,
wawakilishi pamoja na Madiwani.
Nao
wanachama hao wameuomba uongozi CCM kutoka afisi Kuu kufanya ziara za mara kwa
mara ili wananchi wawe na hamasa na viongozi wao wa Chama.


Post a Comment