0
Na. Ahmad Mmow, Lindi.
Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amezitaka kamati za ulinzi na usalama za wilaya mkoani humu pamoja na maofisa ushrika wahakikishe wakulima wa korosho hawadhulumiwi kwa namna yoyote katika msimu huu wa .mwaka 2017/2018.
Zambi alitoa agizo hilo wakati wa kikao cha wadau wa korosho wa mkoa wa Lindi, kilichofanyika leo katika ukumbi wa kituo cha utafiti wa kilimo cha Naliendele uliopo Ngongo, Manispaa ya Lindi. Mkuu huyo mkoa ambae alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho alisema wakulima wamekuwa wakidhulumiwa kwa mifumo na njia mbalimbali nakusababisha kushindwa kupata mapato yanayositahili kulingana na kiasi cha mazao wanayouza. Hivyo kamati za ulinzi na usalama na maofisa wa idara za ushirika wahakikishe wakulima hawadhulumiwi kuanzia katika hatua ya ununuzi hadi malipo.
Zambi aliyeonesha dhahiri kukerwa na dhuluma wanazofanyiwa wakulima kwa kutumia mbinu tofauti katika maeneo tofauti alisema watendaji na viongozi wanawajibu mkubwa wakutanguliza masilahi ya wakulima, badala ya taasisi wanazoongoza au masilahi yao binafsi. Huku akiweka wazi kuwa baadhi ya viongozi na watendaji wa serikali, vyama vya ushirika wanawadhulumu wakulima. “Wanashirikiana na wafanyabiashara wasio waaminifu kuwaibia wakulima, wanatumia udhaifu wabaadhi ya wakulima kutokuwa na elimu. Hiyo haikubaliki nendeni mkasimamie na kuhakikisha hayatokei hayo,”alisema Zambi.
Mkuu huyo wa mkoa ambae nimtaalamu wa ushirika hakuacha kuzitaja badhi ya njia zinazotumika kuwadhulumu wakulima, hasa wa zao la korosho. Ikiwamo baadhi ya watendaji wa vyama vya msingi (AMCOS) kuingiza fedha za baadhi ya wakulima kwenye akaunti zisizo zao (siozawakulima husika), kushirikiana na wezi na majambazi kupanga njama za wizi wa fedha za wakulima, baadhi ya watumishi wa taasisi za fedha kushirikiana na wezi kwa kuwapa namba za siri za akaunti za wakulima. “Baadhi ya watumishi wa benki sio waaminifu, sababu baadhi ya malalamiko ya wizi yanamazingira yanayotia shaka. Mtu anaweka fedha zake halafu anakuta hazipo, fedha ambazo alihangaika mwaka mzima kuzitafuta inauma sana,” Zambi alisema kwa huzuni na kudhihirisha hawapendi watenda dhambi.
Mbali na hayo Mkuu huyo mkoa ame wataka viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) kutopokea korosho za watu wasio na mashamba ya mikorosho. Badala yake washirikiane na serikali kuwabana, kwasababu watu hao watakuwa ni miongoni mwa wanaowadhulumu wakulima.
Ununuzi wa korosho kwa msimu wa 2017/2018 unatarajiwa kuanza tarehe 1 Oktoba, 2017. Ambapo kilo moja ya daraja la kwanza, kwa mujibu wa bei iliyotangazwa na bodi ya zao hilo (CBT) itanunuliwa kwa shilingi 1450.

Post a Comment

 
Top