0
This picture taken on September 23, 2017 and released from North Korea's official Korean Central News Agency (KCNA) on September 24 shows an anti-US rally in Kim Il-Sung Square in Pyongyang.Haki miliki ya pichaKCNA
Image captionKorea Kaskazini yailaumu Marekani kwa kutangaza vita
Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini amedai kwamba rais wa Marekani Donald Trump ametangaza vita dhidi ya taifa hilo.
Ri Yong-ho aliwaambia waandishi wa habari kuwa Korea Kaskazini ina haki ya kudungua ndege za vita za Marekani.
Hi ni hata kwa zile ndege zenye hazipo katika anga ya Korea Kaskazini, aliongeza waziri huyo.
Uwezo wa Makombora ya Korea Kaskazini
Image captionUwezo wa Makombora ya Korea Kaskazini
"Dunia ni lazima ikumbuke kuwa Marekani ndiyo ilikuwa ya kwanza kutangaza vita," Bwana Ri alisema.
Pande hizo mbili zimekuwa zikitupiana maneno makali.
Licha ya majuma kadhaa ya misukusuko, wataalamu wanasema kuwa hakuna uwezekano wa makabiliano ya moja kwa moja kati ya Marekani na Korea Kaskazini.
Baada ya Bw Ri kuhutubia Umoja wa Mataifa siku ya Jumamosi, Rais Trump alijibu kupitia mtandao wa twitter, akisema kuwa Bw. Ri na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un hawatakuwepo kwa muda ikiwa wataendelea na maneno yao.
Jibu la Bwana Ri lilikuja wakati akiondoka New York baada mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa.
Makombora ya Hwasong yakiwa katika maonyeshoHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMakombora ya Hwasong yakiwa katika maonyesho
Korea Kaskazini imeendelea na majaribioya makombora ya nyuklia na ya masafa marefu siku za hivi karibuni licha ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
Viongozi wa nchi hiyo wanasema kuwa uwezo wake wa zana za nyulia ndiyo njia pekee dhidi ya mataifa yanayotishia kuiharibu.
Baada ya jaribio la hivi majuzi na kubwa zaidi la nyulia mapema mwiezi huu, baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, liliidhinisha vikwazo vipya dhidi ya nchi hiyo

Post a Comment

 
Top