0

Habari ni kuwa Klabu ya Njombe Mji ambayo inashiriki Ligi Kuu Bara haitaendelea kuwa na kocha wake mkuu, Hassan Banyai baada ya mkataba wake kusitishwa kutokana na matokeo mabaya katika mechi tatu za mwanzo za ligi hiyo.

  
Njombe Mji FC imefungwa mechi zote tatu za mwanzo za Ligi Kuu Bara, mbili nyumbani kwenye Uwanja wa Sabasaba dhidi ya Tanzania Prisons 2-0 na Yanga 1-0 kabla ya kuchapwa 1-0 na Mbeya City Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. 

Kabla ya kuingia kwenye mchezo wa nne dhidi ya Ruvu Shooting mnamo Septemba 23, mwaka huu, klabu hiyo ya Njombe Mji imetoa taarifa ya kutengana na kocha wake huyo aliyeipandisha timu Ligi Kuu msimu huu. 

Ofisa Habari wa Njombe Mji FC, Solanus Mhagama amesema kwamba kwa kipindi hiki, aliyekuwa Kocha Msaidizi, Mrage Kabange ndiye ataiongoza timu hadi hapo uongozi utakapotoa tamko lingine. 

Aidha, Njombe Mji imemshukuru Banyai kwa mchango wake kwenye timu ikiwemo kuipandisha Ligi Kuu na kumtakia kila la heri huko aendako.

Post a Comment

 
Top