Mpaka dakika 90 za mchezo.
Mnamo
kipindi cha pili mchezaji wa timu ya Serengeti Boys,Issa Abdi Makamba
anaipatia goli la 3 dhidi ya timu ya Congo Brazzaville.Mpaka mpaka
dakika 90 za mchezo,timu ya Serengeti Boys wameibuka washindi kwa
kuiburuza timu ya Congo Brazzavile 3-2 ,uwanja wa Taifa jijini Dar.
Timu ya Serengeti Boys (Tanzania),katika kipindi cha kwanza ilikuwa ikiongoza goli 2-0 ,ambapo mnamo dakika ya 40 na 42 mchezaji Yohana Oscar Mkomola aliipatia timu yake magoli mawili dhidi ya timu ya Congo Brazaville,katika mchezo unaonendelea hivi sasa katika uwanja wa Taifa jijini Dar,ambapo Brazzaville wamejipatia goli la pili kipindi cha pili.Serengeti boys wameifunga Congo Brazzavile goli 3-2 dhidi ya Congo Brazzavile,goli la tatu limefungw na mchezaji Issa Abdi Makamba.
Mashabiki wakimshangilia mchezaji wa timu ya Serengeti Boys,Yohana Oscar Mkomola mara baada ya kufungua goli la pili dhidi ya timu ya Congo Brazzaville.
Mchezaji wa timu ya Congo Brazzaville Ngumbi Exau akiruka hewani kumzuia mchezaji wa timu ya Serengeti Boys Yohana Oscar Mkomola asiondoke na mpira.
Katika kipindi cha kwanza kila timu ilionesha kiu kubwa ya kutaka kupata magoli mapema,kila timu ilikuwa ikishambulia lango la mwenzake kwa spidi kubwa,mpaka dakika 90 za mchezo timu ya Srengeti Boys imeibuka kwa ushindi wa goli 3-2 dhidi ya Congo Brazzavile.









Post a Comment