0


KAMPUNI ya Puma Enegy Tanzania, imehitimiza mashindano ya uchoraji picha za usalama barabarani kwa shule za Msingi kwa mwaka 2017 kwa kutoa kutoa zawadi ya Sh milioni 2 kwa mshindi wa kwanza. 

Akizungumza jijini Dar e Salaam jana Mkurugenzi Mkuu wa Puma Enegy Tanzania Ltd, Philippe Corsaletti, alisema kuwa mashindano ya mwaka huu yalihusisha jumla ya shule 14 za mikoa ya Dar es Salaam na Kilimanjaro ambapo washindi hao walipatikana jana. 

Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza aliyeibuka ni Nasri Mwema wa Shule Msingi Amani katika shindano hilo lililoshirikisha shule 14. 

“Mshindi huyu wa kwanza atapata kikombe na cheti ambapo shule anayotoka itapata fedha Shilingi milioni 2 ambazo zitatumika kwa ajili ya kununulia vitabu. Shindano hili la usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi kwa njia ya uchoraji linalenga kusaidia kuelimisha wanafunzi wa shule za msingi katika masuala ya usalama barabarani. 

“Mpango wetu wa usalama barabarani kwa shule hapa nchini Tanzania ulianza tangu mwaka 2013 na mpaka sasa shule za msingi zipatazo 47 zimeshashiriki zikiwa na jumla na wanafuzni 60,000 kutoka mikoa mbalimbali,” alisema Corsaletti 

Mkurugenzi huyo wa Puma Enegy, alisema kuwa shindano hilo la usalama barabarani kwa njia ya uchoraji linalenga kumpatia kila mwanafunzi nafasi ya kushirikisha mawazo yake juu ya namna bora ya kuboresha usalama barabarani ambapo kati yao huchaguliwa washindi na kuzawadiwa. 

“Lengo letu la muda mrefu ni kufikia shule zote hapa nchini ziweze kushiriki katika mpango huu. Kampuni ya Puma Enegy imekuwa ikishirikiana kwa karibu na Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani pamoja na SUMATRA katika masuala mbalimbali yahusuyo usalama barabarani. 

“Tunaamini kwamba ajali za barabarani zinaweza kupungua kwa kiasi kikubwa ikiwa pande zote zinazohusika ambazo ni pamoja na madereva, wenye magari na wasimamizi wakitekeleza wajibu wao ipasavyo. Jukumu letu pamoja linabaki kuwa wajibu shirikishi katika kutengeneza mazingira salama kwa ajili ya watoto wetu na vizazi vijavyo,” alisema alisema 

Naye Msajili wa Hazina, Dk. Osward Mashindano, alisema kilichofanywa na Kampuni ya Puma ni jambo jema ambalo litasaidia katika kuiandaa jamii kuepuka ajali za barabarani.

Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu (kushoto), akimwangalia Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Amani, Nasri Mwema baada ya kumkabidhi tuzo ya kuwa mshindi wa kwanza kwa kuchora vizuri picha inayoelezea athari za usalama barabarani katika hafla iliyoandaliwa na Kampuni ya Uuuzaji Mafuta ya Puma Energy katika Shule ya Msingi Diamond Dar es Salaam leo. Mashindano hayo yanadhaminiwa na Puma Energy Tanzania. Kulia ni Msajiri wa Hazina, Oswald Mashindano na Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Phillipe Corsaletti. 

Mwanafunzi Nasri Mwema akipokea tuzo kutoka kwa Msajiri wa Hazina , Oswald Mashindano (kulia),.Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Puma, Phillipe Corsaletti.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Puma, Phillipe Corsaletti akipongezana na Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu 
Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu na viongozi wengine wakishiriki kuteua picha bora tatu zilizochorwa na wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi Mkoa wa Dar es Salaam.
Mwanafunzi George Jonas wa Shule ya Msingi Upendo akikabidhiwa begi na madaftari yenye alama za usalama barabarani baada ya kuwa mshindi wa tatu katika mashindano hayo
Mshindi wa pili wa shindano la uchoraji wa picha za kuonesha athari za usalama barabarani, Rehema Mzimbili wa Shule ya Msingi Buza, Temeke, Dar es Salaam, akipokea vifaa vyake vya shule.
Mshindi wa Kwanza Nasri Mwema akiwa katika picha ya pamoja na viongozi  baada ya kukabidhiwa zawadi ambapo pia Shule yake ya Amani ilizawadiwa  sh. mil. 2.
Kamanda Musilimu akionesha picha iliyoshinda katika mashindano hayo
Washindi kwakiwa katika picha ya pamoja

Post a Comment

 
Top