0


Baadhi ya wakulima wa zao Korosho  mkoani  Lindi  wanaiomba serikali izuie mpango wa Halmashauri za  wilaya kutoza ushuru kupitia bei ya sokoni badala ya bei dira iliyotangazwa na bodi ya zao hilo (CBT)

Akizungumza  kwa  niaba  ya  wakulima  hao  Rashid Kassim  alisema serikali haina budi kuzibana Halmashauri  za  mkoa   wa  Lindi kuto  katwa  ushuru  kwa  bei  ya sokoni Kwani zikiachwa zitoze kupitia bei hiyo  badala ya bei dira, itakuwa  serikali imeshindwa  kutimiza lengo  la kuwasaidia  wakulima

 Rajabu Ngwani,Aliomba  serikali izibane Halmashauri isitekeleze mpango wa kuchukua 3% kama katika kilo moja ya bei ya kuuzia badala ya shilingi 1450 iliyotangazwa na bodi ya korosho kama bei dira.7:Ngwani alisema Halmashauri zisilazimishe kupata au kuvuka 80% ya mapato yake ya ndani kupitia ushuru wakorosho peke yake.

"Halmashauri ni zetu sisi zisijifanye zipo juu ya wananchi.Kama serikali kuu imeona iwasaidie wananchi kwanini halmashauri ziende kinyume.Iwapo kweli serikali ilikuwa na nia njema izizue halmashauri,vinginevyo yenyewe itabeba lawama, "alishauri na kuonya Ngwani.

Mkulima Mussa Mkoyage wa Liwale alisema dhamira ya serikali kuondoa baadhi ya tozo kwenye mazao ya kilimo ni kutaka kuwainua wakulima.Huku akibainisha kuwa hata halmashauri zilikuwa zinatoza 5% zimetakiwa kutoza 3%.Nia ni kuwasaidia wakulima.

Hivyo Halmashauri zikiachwa zifanye zinavyotaka, wakulima wataumia sana.Mkoyage alisema hadi sasa thamani ya tozo zitazo tozwa katika wilaya hiyo kutoka kwenye zao hilo itafikia shilingi 250,iwapo tozo zote zitaruhusiwa kwa kingizio cha mchango. 
Ingawa serikali ilipunguza kutoka shilingi 260 nakufikia shilingi 130 baada ya kuondoa baadhi ya tozo.
Ahmad Ngayetuka, aliyesema wakulima wa zao hilo wamesitushwa na kuchanganyikiwa baada ya kusikia mpango huo wa halmashauri.

Bakari Mawata,alisema halmashauri zinahaki ya kupata ushuru kwa ajili ya shuguli za maendeleo. Hats hivyo isilazimshe chanzo kimoja kitengeneze na kukamilisha makisio yamapato yake ya ndani.chanzo,sautiyakusini.com

Post a Comment

 
Top