Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Liwale mkoani Lindi,Dr. Maulid Majala akizungumza leo septemba 14 kwenye tamasha la malaria lilofanyika stendi kuu ya mabusi wilayani hapa.
Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Liwale mkoani Lindi,Dr. Maulid Majala amewataka wananchi wilayani hapa kuwaamini wataalum wa afya wanapotoa majibu mara baada ya kufanyiwa vipimo vya Malaria na kusema sio kila homa ni malaria.
Dr. Majala ameyasema ayo leo septemba 14 kwenye ufunguzi wa tamasha la malaria lililofanyika viwanja vya stendi kuu ya mabasi wilayani hapa .
Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Liwale,Damas M. Mumwi aliwasisitiza wananchi wanapogundulika kuwa na homa ya malaria baada ya kupatiwa vipimo kutoka kwa madaktari ni vema wakazingatia matibabu ya wataalam na kumaliza dozi wanazopatiwa.
Tamasha hilo la Malaria mwaka huu likiwa limebeba kauli mbiu isemayo “Zama zimebadilika sio kila homa ni malaria”
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Liwale,Damas M. Mumwi(kushoto )akizungumza kwenye tamasha la malaria leo septemba 14
Wananchi wa wilaya ya Liwale walioudhulia kwenye tamasha la malaria akifuatilia kwa umakini maelezo mbalimbali kutoka kwa watalaam
Wananchi wa wilaya ya Liwale walioudhulia kwenye tamasha la malaria akifuatilia kwa umakini maelezo mbalimbali kutoka kwa watalaam
Kikundi cha burudani kikitoa burudani kwa wakazi wa wilaya ya Liwale kwenye tamasha la malaria
Wananchi wa wilaya ya Liwale walioudhulia kwenye tamasha la malaria akifuatilia kwa umakini maelezo mbalimbali kutoka kwa watalaam
Burudani mbalimbali ziliweza kuburudisha watu waliokuja kusiliza ujumbe muhimu wa malaria
Wasanii nao hawakuachwa waliweza kupewa nafasi za kutoa burudani kwa wananchi waliokuja kwenye tamasha la malaria
Wasanii wa Liwale nao walipewa nafasi ya kutoa burudani ikiwemo msanii Magwala boy hapo juu na Man mbawa waliweza kutoa burudani
Msanii Man mbawa akitumbuiza kwenye tamasha la malaria lilofanyika leo wilayani Liwale
Post a Comment