Mkoa wa Lindi ni miongoni mwa mikoa yenye tatizo la utapiamlo kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano takwimu zinaonesha kwamba kiwango cha udumavu katika mkoa wa Lindi ni asilimia 44, hali inayoashiria kwamba katika kila kundi la watoto kumi wenye umri chini ya miaka mitano, watoto watano wamedumaa.
Tatizo hili linarudisha nyuma maendeleo ya mkoa na taifa kwa kiasi kikubwa, hali hii inapelekea kutokufikia kwa malengo ya dira ya maendeleo ya taifa kwani athari zinazotokana na tatizo la Utapiamlo ni watoto kuugua uzito mara kwa mara vifo na ukuaji duni kimwili na kiakili.
Moja ya sababu kubwa inayochangia tatizo la utapiamlo katika mkoa wa Lindi ni kukosekana kwa elimu sahihi kuhusu umuhimu wa lishe ya watoto wachanga na wadogo pia kuto kutambua umuhimu wa lishe kwa wanawake wajauzito na baada ya kujifungua,na kuendeleza mila na desturi zilizopitwa na wakati ikiwemo ya kukamulia maziwa ya awali ya mama kwenye figa kwa madai machafu na kuwalisha watoto vyakula kabla kufikia umri wa miezi sita.
Kwa kutambua ukubwa wa tatizo hilo la kukosa elimu ya lishe kwa watoto na wanawake mashirika yasio ya kiserikali ya ROWODO na ROPA yanajitolea kutoa elimu ya lishe ngazi ya kaya, na jamii kwa njia ya Sanaa kupitia Mradi wa lishe wa HANO (Harnessing Agriculture for Nutrition Outcomes) kwa kushirikiana na Shirika la Save the Children International
Kwenye kampeni hiyo wadau mbalimbali wa maendeleo ya mtoto walionyesha hisia na kukerwa kwa baadhi ya tabia, mila na desturi zinazoendekezwa na wazazi,
Habiba Poza mkazi wa kijiji cha Kiwalala alisema serikali na wadau wa maendeleo wanatakiwa kujikita zaidi kutoa elimu, kwani elimu inayotolewa ni ndogo ikilinganishwa ma kiwango cha imani, mila na desturi walizonazo wananchi.
Poza alisema kuna haja kubwa ya serikali na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kuendelea kutoa elimu kama wanavyofanya Asasi ya ROWODO kwani ni watu wachache wenye uelewa kuhusu lishe ya mtoto na mama mjamzito, I ngawa vyakula vyote vinapatikana kwenye maeneo wanayoishi, ikiwemo mboga za majani, mayai, nyama na chumvi yenye madini joto.
Mariamu Saidi mkazi wa majengo Mtama alisema idadi ya wanaoamini mila na desturi potofu bado kubwa ikiongozwa na wanaume kutokana na kujiona wana haki zaidi na kuwaona wanawake kama watumishi wao.
Mariamu alisema kutokana na hali hiyo wanaume wengi wamewaachia wanawake suala la malezi ya watoto na wakati mwingine wamekuwa wakiwazuia wasiudhurie kliniki wakati wa ujauzito baada ya wakijifungua.
Alisema kwa elimu ndogo na umasikini unasababisha kuendeleza mila na desturi ya kukamulia maziwa ya awali ya mama kwenye figa na kuwalisha watoto vyakula kabla kufikia umri wa miezi sita.
Saidi Ngwinde mkazi wa Mbekenyera wialaya Ruangwa aliongeza kuwa suala la Kukumbatia mila potofu na uelewa mdogo juu ya masuala ya ya lishe bora kwa watoto na wamama wajawazito limekuwa tatizo kubwa kwa jamii ya wakazi wa wilaya hiyo
Alisema serikali na wadau wanawajibu mkubwa kutoa elimu kuhusiana na lishe kwani niwatu wachache wenye ufahamu kuhusu lishe ya mtoto Ikiwamo umuhimu wa chumvi iliyowekwa madini joto Ngwinde, alisema elimu ndogo na umaskini unasababisha watu kuendekeza mila na desturiza kuwalisha watoto vyakula kabla ya kufikisha muda wa miezi 6.Meneja wa shirika la save the children mkoa wa Lindi Nengilanget Kivuyo alisema suala la lishe, katika mkoa wa Lindi lina changamoto nyingi zinazopelekea ulishaji watoto na wajawazito kutokutekelezeka ipasavyo kutokana na dhana potofu kuhusu maziwa ya mama ya mwanzo baada ya kujifungua, ikiwemo kukamua maziwa ya mwanzo na kuyamwaga kwa kufikiria ni machafu na kumkosesha mtoto maziwa ambayo ni bora na yenye virutubishi vingi na kinga kwa Afya na ukuaji wake.
Kivuyo aliongeza kuwa Kuwalimbikizia kazi ngumu a kina mama wanaonyonyesha kama vile kulima, kuchota maji, kukata kuni, kupika, kufua, kutwanga hali inayopelekea mama anayeyonyesha kukosa muda wa kupumzika na kuwa karibu na mwanae ili kuchochea tendo la unyonyeshaji na Wanawake walio wengi hasa walio watumishi katika Taasisi za umma na zisizo za kiselikali hawafahamu vizuri haki ya uzazi katika sheria mpya ya kazi Na. 6 ya Mwaka2004, hali ambayo inapelekea kushindwa kudai haki zao kipindi cha ujauzito na baada ya kujifungua.
Alisema hali duni ya kiuchumi kwa kina mama walio wengi inapelekea kina mama wengi kuachisha kunyonyesha watoto wao mapema na kwenda kutafuta riziki Wanawake wengi kutokuwa na Elimu ya kutosha kuhusu umuhimu wa maziwa ya mama na namna ya kunyonyesha watoto wao,Ushiriki mdogo wa baba na wanafamilia wengine katika kuweka mazingira mazuri ya uwepo wa lishe bora kwa mama mja mzito, mama anaenyonyesha na kwa watoto wadogo na wachanga.
Nae mkurugenzi wa Asasi ya ROWODO Scolastica Nguli alisema kampeni hiyo maalum ya lishe inayotumia Sanaa yenye kuchochea majadiliano juu ya hali ya lishe ni mwendelezo wa elimu inayotolewa na mradi katika ngazi ya jamii na kaya juu ya ulishaji sahihi kwa watoto wadogo na wachanga ikiwemo unyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee kwa watoto wenye umri chini ya miezi sita, ulishaji sahihi wa vyakula vya nyongeza kwa watoto wenye umri zaidi ya miezi sita, pamoja na matumizi ya chumvi yenye madini joto, vidonge vya kuongeza damu kwa watoto na akina mama wajawazito.
Nguli alisema tatizo la madini joto katika Mkoa wa Lindi ni kubwa sana, kutokana na takwimu za mwaka 2010 mkoa wa Lindi ni asilimia 6 tu ya kaya hutumia chumvi zenye madini joto kwa mama wajawazito ni muhimu sana kwani huzuia kuharibika kwa mimba,hupunguza uwezekano wa kuzaa watoto wenye mtindio wa ubongo na hupunguza uwezekano wa kuzaa mtoto mfu.
Alisema kazi zote zilizofanyika katika kampeni ya unyonyeshaji,watoa huduma walitoa ushauri wa matumizi ya chumvi zenye madini joto kwa mama wajawazito na jamii kiujumla pamoja na namna ya kuzihifadhi chumvi zenye madini joto, kuhakikisha elimu juu ya lishe bora kwa mama wajawazito, akina mama wanao nyonyesha na watoto wadogo na wachanga inawafikia wajamii wote na wadau mbalimbali wa lish
Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Joseph Mkirikiri hali ya Lishe katika Taifa letu na Mkoa wetu wa Lindi bado ni tatizo kubwa. Kama takwimu za mwaka 2015/16 zinavyoonyesha, Kitaifa watoto wenye udumavu ni asilimia 34 wakati kimkoa hapa Lindi ni asilimia 44, tumevuka hata asilimia za kitaifa, hii inaashiria kwamba katika Mkoa wa Lindi tatizo la utapiamlo ni kubwa sana.
Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Joseph Mkirikiri hali ya Lishe katika Taifa letu na Mkoa wetu wa Lindi bado ni tatizo kubwa. Kama takwimu za mwaka 2015/16 zinavyoonyesha, Kitaifa watoto wenye udumavu ni asilimia 34 wakati kimkoa hapa Lindi ni asilimia 44, tumevuka hata asilimia za kitaifa, hii inaashiria kwamba katika Mkoa wa Lindi tatizo la utapiamlo ni kubwa sana.
Mkirikiti alisema ukweli usiopingika jamii bado inahitaji elimu zaidi kuhusiana na Lishe bora na kubadili mtindo wa maisha ili waweze kubadilika na kuwa na Taifa lenye watu wenye afya nzuri na fikra nzuri na kuweza kufanya kazi za maendeleo ili kuongeza vipato vyao na uchumi wa Taifa kiujumla.
Alisema maafisa Lishe wasichoke kuelimisha jamii umuhimu wa Lishe bora hususan katika siku 1000 za mwanzo kuanzia kutunga mimba hadi mtoto anapofikisha miaka miwili, kipindi hiki ni hatari sana endapo mama mjamzito na mwanae aliye tumboni hawatapata Lishe bora kwani mtoto anaweza kudumaa kuanzia tumboni mwa mama yake.
“Ndugu zangu naomba niwakumbushwe kuwa tukishindwa kuwapa malezi kipindii hiki mtoto akidumaa hali hii haiwezi kurekebishika tena hivyo itapelekea kwa miaka ijayo kuwa na watu waliodumaa kiafya na kiakili”. Alisema Mkirikiti
alisema tatizo la madini joto katika mkoa wetu wa Lindi ni kubwa mno kama takwimu za mwaka 2010 zinavyoonyesha ni asilimia 6 tu ya kaya zinatumia chumvi zenye madini joto ni muhimu sana katika ukuaji wa kiakili kwa watoto wetu,hali kadhaalika kwa mama mjamzito.
Alisema kitendo cha mkoa wetu wa Lindi ukishika nafasi ya mwisho katika mitihani mbalimbali ya kitaifa shule ya msingi na sekondari,ufaulu wa watoto upo chini sana hii inachangiwa na ukosefu wa madini joto kwa mtoto tangu tumboni mwa mama yake.
Mkirikiti alisema uwepo wa madini joto mwilini husaidia utengenezwaji wa ubongo na kuongeza uwezo wa kiakili kwa binadamu lakini hili huanza kufanyika tangu kutungwa kwa mimba hivyo ni vema tukatumia chumvi zenye madini joto ili kuhakikisha tupata watoto wenye uwezo mkubwa kiakili.

Post a Comment